27.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 17, 2024

Contact us: [email protected]

Ajali ya basi yaua mmoja, yajeruhi 46

NA ABDALLAH AMIRI, IGUNGA

MTU mmoja, amefariki dunia papo hapo na wengine 46 kujeruhiwa vibaya baada ya basi la Kampuni ya ALLY’S lenye namba za usajili T 560 AKW aina ya Scania, kupinduka katika Kijiji cha Igogo, Kata ya Nanga, Wilaya ya Igunga, mkoani Tabora.

Ajali hiyo ilitokea jana, saa 12 alfajiri wakati basi hilo lilipokuwa likitoka wilayani Igunga kwenda jijini Mwanza.

Wakizungumza na MTANZANIA eneo la tukio baada ya ajali hiyo, mmoja wa abiria aliyenusurika, Emmanuel Julius (32), alisema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi lao kutaka kulipita lori la mizigo lililokuwa mbele yao.

“Ajali ilisababishwa na dereva kwani alipotaka kulipita roli lililokuwa mbele yetu, gari lilimshinda na kuacha barabara kabla halijapinduka na kuviringika mara tatu.

“Kwa hiyo, naamini kama dereva wetu angekuwa makini, ajali hii isingetokea hapakuwa na sababu ya kulipita roli hilo la mizigo,” alisema Julius.

Kwa upande wake, Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Godfrey Mgongo, alithibitisha kupokea mwili wa mtu mmoja alimyemtaja kwa jina la Denis Nsokolo (54), mkazi wa Igunga mjini.

Pamoja na mwili huo wa marehemu, Mgongo alisema alipokea majeruhi 46 wakiwamo wawili waliohamishiwa katika Hospitali ya Nkinga kwa ajili ya matibabu zaidi.

Aliwataja majeruhi walioamishiwa katika Hospitali ya Nkinga kuwa ni dereva wa basi hilo, Mohamed Yusuph ambaye amevunjika mfupa wa paja abiria Michael James.

“Waliopewa rufaa ya kwenda Nkinga ni hao lakini waliobaki wanaendelea na matibabu kwa sababu hali zao siyo mbaya sana,” alisema Mgongo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Hamis Seleman hakupatikana ili kuthibitisha ajali hiyo kwa kuwa simu yake ya mkononi haikuwa hewani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles