27.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 17, 2024

Contact us: [email protected]

Tanasha wa Diamond mjamzito?

Bethsheba Wambura, Dar es Saalaam

Mchumba wa Mwanamuziki Nasib Abdul maarufu Diamond , Tanasha Donna huenda akawa mjamzito baada ya kutuma kipande cha video katika mtandao wa Instagram huku tumbo likionekana kubwa tofauti na alivyokuwa awali na kupelekea watu kuhisi pengine wawili hao wanatarajia mtoto hivi karibuni.

Katika video hiyo Tanasha ambaye ni raia wa Kenya pia ni msanii na mtangazaji wa radio moja nchini humo, aliyoituma Instagram jana Juni 9, wawili hao wanaonekana wakicheza wimbo wa Inama ambao Diamond ameimba kwa kushirikiana na msanii kutoka nchini Congo, Fally Ipupa.

Hivi karibuni kumekuwepo na maoni ya watu tofauti katika mitandao mbalimbali ya kijamii wakisema huenda Tanasha akawa mjamzito baada ya  picha anazotuma mitandaoni hivi karibuni kumuonesha akiwa na tumbo kubwa linaloonesha kukua siku baada ya siku.

Japo wenyewe hawajathibitisha, endapo ikiwa ni kweli basi Diamond atakuwa anatarajia mtoto wa nne ikiwa anao watatu tayari ambapo  wawili (Latifa na Neelan) alizaa na Mwanamama Zarina Hassan ambaye ni raia wa Uganda na mtoto mmoja wa kiume (Dylan), aliyezaa na mrembo wa hapa nchini Hamisa Mobetto.

Aidha wawili hao walianza mahusiano yao Desemba mwaka jana kwa kuweka wazi kupitia mitandao ya kijamii na Januari 13, mwaka huu Diamond alimtambulisha rasmi Tanasha kwa mama yake mzazi Sanura Kassim maarufu Sandra.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles