Tamasha la vyakula na vinywaji vya asili kufanyika Dar mwezi huu

0
1335

vyakula

Katika kuhakikisha kuwa vyakula na vinywaji vya asili vinaenziwa na kutangazwa kitaifa na kimataifa, kumeandaliwa tamasha la Vyakula na Vinywaji ili kutimiza hilo.

Tamasha hilo lilopewa jina la Pepsi Dar es Salaam Food and Drink Festival, litafanyika Octoba 8 mwaka huu katika viwanja vya Leaders Club, Dar es Salaam.

Waandaaji wa tamasha ambao ni Kampuni ya EM & U Investment wakishirikiana na SBC Ltd, wamesema litahusisha burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali nchini pia wale wa kigeni kutoka China, India, Italy, Mexico, Ufaransa na Japan.

Mbali na burudani kutakuwa na upimaji afya bure wa magonjwa ya moyo na kisukari pia kutoa ushauri bure.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here