Waziri Mbarawa aiagiza TEMESA kuongeza mapato ya vivuko Dar

0
752

mbarawa

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameuagiza uongozi wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA), kuhakikisha wanaweka mipango madhubuti ya kuongeza mapato katika vivuko vya MV. Kigamboni na MV. Magogoni kutoka Shilingi Milioni 14 ambazo zinakusanywa hivi sasa hadi kufikia Milioni 19 kwa siku.

kigamboni

Akizungumza jijini Dar es Salaam mara baada ya kukagua vivuko hivyo na kuongea na Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dk. Mussa Mgwatu, Profesa Mbarawa alisema kuwa kipimo cha utendaji huo utafanyika ndani ya miezi minne ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wa vivuko hivyo na kuweza kufikia malengo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here