26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

Tamasha la Pasaka kufanyika Aprili 9, Leaders, hakuna kiingilio

*…litatumika pia kumuombea Rais Dk. Samia

Na Beatrice Kaiza, Mtanzania Digital

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa matamasha mbalimbali ya Injili nchini, Alex Msama amesema Tamasha la Pasaka mwaka huu litakuwa la kihistoria na kufanyika bure.

Amesema tamasha litafanyika katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni jijini Dar es Salaam na kwamba hakutakuwa na kiingilio, litakuwa ni buree.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 23, 2023 kwenye Ofisi za Kampuni hiyo zilizopo Kinondoni jijini Dar es Salaam, ambapo amesema kuwa waimbaji mbalimbali kutoka Tanzania na nchi za Afrika Mashariki watatumbuiza.

Rais Samia Suluhu Hassan.

“Maandalizi ya tamasha la Pasaka yanaendelea vizuri, hapo awali tamasha letu lilitakiwa lifanyike uwanja wa Taifa, lakini kwa sababu zilizo nje ya uwezo wetu tamasha hili halitafanyika tena Uwanja wa Taifa na badala yake litafanyika katika viwanja vya Leaders club, kwa hiyo tamasha lipo kama kawaida Aprili 9,2023 na mpaka sasa waimbaji wengi wamethibitsha kushiriki,” amesema Msama.

Aidha, amesema kuwa tamasha hilo pia litakuwa la kumshukuru Mungu katika kusherehekea miaka miwili ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan na kwamba watatumia nafasi hiyo kumuombea ili aendelee kuiongoza nchi ya Tanzania kwa amani.

“Tamasha letu pia ni la kumshuru Mungu kwa ajili ya uongozi wa mama yetu, Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza miaka miwili madarakani kwa mafanikio makubwa, miradi mingi imeendelea, kila kitu kinaenda vizuri, tunaishi kwa amani na utulivu hivyo ni lazima tumshukru Mungu kwa uongozi wa Rais wetu,” ameongeza Msama.

Aidha, aliongezea kuwa baadhi ya waimbaji watakaoshiriki kwenye tamasha hilo ni
Upendo Nkone na Mwakilishi wa kundi la Zabron Singers Emmanuel Zabron na wengine wengi

Kwa upande wa mratibu wa Tamasha la Pasaka, Emmanuel Mabisa amesema kuwa mpaka sasa waimbaji wote walioalikwa kushiriki kwenye Tamasha hilo wamethibitisha ushiriki wao na kwamba maandalizi yote yanaenda vizuri.

“Tamasha lililokuwa likisubiriwa kwa miaka mingi la Pasaka nimewadia na itafanyika katika viwanja vya Leaders Club bure bila kiingilio, hivyo wananchi wasisite kutoka na familia zao kuhudhuria kwenye tamamsha hilo vyakula na vinywaji vitakuwepo kwa bei nafuu,” amesema Mabupa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles