30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Samia ana nia njema na vyombo vya habari, nchi-Balozi Boer

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

“Nampongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan wa kufungua milango katika utendaji kazi wa vyombo vya habari Tanzania, vyombo vya habari sasa visiwe vioga katika kutekeleza majukumu yake. Ameonesha namna anavyohitaji vyombo hivyo kuwa huru, wanahabari nao watumie nafasi hiyo kuimarisha uhuru wao,” Balozi Boer.

Ni kauli ya Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Wiebe de Boer ambaye amempongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha utendaji kazi wa vyombo vya habari nchini na kwamba, ameonesha mfano bora.

Balozi Boer ametoa kauli hiyo juzi alipokutana na viongozi wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), katika ofisi za ubalozi huo, jijini Dar es Salaam.

Amesema katika hatua nyingine Balozi Boer huyo amesema, Rais Samia amefanya jambo kubwa kwa kuunganisha umoja hasa kwa kushirikiana na vyama vya upinzani katika mambo mbalimbali.

“Jambo analofanya Rais Samia ni la kupongezwa, hatua ya kushiriki kwenye mikutano ya vyama vya upinzani, inaonesha kwa kiwango kikubwa anataka kuunganisha nchi.

“Hii ni fursa ya kujenga nchi moja na kushirikiana kujenga uchumi imara. Ni vizuri kwa sasa na vyombo vya habari visiogope kufanya kazi na vyama vya upinzani kwa kuwa hata rais kaonesha kwamba hakuna tatizo,” amesema Balozi Boer.

Pia amelipongeza Jukwaa la Wahariri Tanzania na wadau wa habari kwa kuonesha mshikamano katika kupigania uhuru wa habari na kwamba, jambo lolote huenda taratibu mpaka linafanikiwa.

Deodatus Balile, Mwenyekti wa TEF amempongeza Balozi Boer kwa nchi yake kuwa karibu na vyombo vya habari Tanzania.

Hata hivyo, amemhakikishia kwamba vyombo vya habari vya Tanzania vinatarajia kuwa na sheria inayokuza tasnia ya habari na si inayoweka vikwazo vinavyoweza kuua kabisa thamani ya tasnia hiyo.

“Tuna imani na mchakato wa mabadiliko ya sheria ya habari, rais na serikali yake alionesha mapema nia ya kuondoa vikwazo katika uhuru wa habari nchini kwetu. Ndio maana maana baada ya kuingia madarakani alianza kufungulia vyombo vilivyokuwa vimefungwa ambavyo ni MwanaHalisi, Mawio, Raia Mwema na Tanzania Daima pamoja na Televisheni za mtandaoni.

“…lakini hata katika Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Habari, kuna vikwazo vimeondolewa ikiwa ni pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maeleza kupunguziwa mamlaka,” amesema Balile.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles