23.8 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

TAMA: Serikali iwekeze zaidi kwa wakunga kuokoa maisha ya mama na mtoto

*Yaomba Serikali iajiri zaidi wakunga

Na Faraja Masinde, Mtanzania Digital

Serikali imetakiwa kuwekeza zaidi kwa Wakunga ili kuokoa maisha ya kina mama wajawazito wakati wa kujifungua pamoja na watoto.

Wito huo umetolewa leo Dar es Salaam Aprili 28, 2022 na Rais wa Chama cha Wakunga nchini(TAMA), Feddy Mwanga, kwenye kikao na waandishi wa habari kuelekea siku ya wakunga duniani Mei 5, ambayo kitaifa itafanyika mkoani Dodoma Mei 7, ikiwa na kauli mbiu ya Wekeza kwa Mkunga, Okoa maisha.

Kaimu Mwakilishi Mkazi wa UNFPA), Dk. Wilfred Ochani, akifungua mkutano huo.

Amesema kuwa kwa dunia nzima ripoti zinaonyesha kuwa kuna uhaba wa wakunga 900,000 na kwamba iwapo jitihada zitafanyika kiwango hicho kinaweza kupungua.

“Takwimu zinaonyesha kuwa uhaba wa Wakunga Tanzania ni asilimia 52, lakini kwa duniania nzima upungufu ni wakunga 900,000 na iwapo jitihada zitafanyika basi inaweza kupunguza pengo hiki hadi kufikia 750,000 kufikia mwaka 2030.

“Hivyo ifahamike kwamba kama tutawekeza vizuri kwa Wakunga wanaweza kuokoa vifo milioni 4.2 vya akina mama ifikapo mwaka 2035, kwani wanaweza kufanya kazi kwa asilimia 90 katika afya ya uzazi kwa kina mama na watoto wadogo, kwani pia mkunga anajukumu la kuhakikisha kuwa wote wawili wanakuwa salama,” amesema Feddy.

Ameongeza kuwa jitihada nyingi zimeendelea kufanyika katika kuhakikisha kuwa idadi ya wakuunga inaongezeka ikiwamo kufikia maeneo ya vijijini ili kuokoa maisha.

“Wakunga wamekuwa wachache sana na hata wenye ujuzi bado hawatoshelezi, kama tunavyojua kuwa vifo vya kina mama vitokanavyo na uzazi bado ni changamoto katika nchi yetu na imedhihirika kuwa bado kuna umuhimu wa wakunga. Hivyo Vyombo vya habari mna mchango mkubwa wa kuhakikisha kuwa mnafikisha ujumbe huu.

“Juhudi zaidi zinafanyika kuhakikisha kuwa wakunga wanaoajiriwa wanaenda vijijini, ajira nyingi zinapitia kwa wakurugenzi na ndiyo maana wanajitahidi kuwavuta kwenye maeneo ya vijijini kwa kuwapatia nyumba za kukaa,” amesema.

Upande wake, Felista Bwana kutoka Shirika la Umoja wa Taifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi (UNFPA), amesema lengo la siku hiyo ni kukumbuka mchango wa Wakunga katika kuimarisha afya ya uzazi kwa kina mama na watoto.

“Wakunga wamekuwa na mchango mkubwa katika kutoa huduma bora wakati wa uzazi na ndio maana tumekuwa hapa kwa ajili ya kuwakumbusha mchango wa wakunga nchini.

“Hivyo kuelekea maadhimisho hayo, yatatanguliwa na mkutano wa Kisayansi wa siku mbili wa tarehe 5 na 6 kabla ya kilele ambapo hapa kwetu itakuwa tarehe 7 mkoani Dodoma kutokana na mwingiliano wa shughuli,” amesema Felista na kuongeza kuwa wanawake wengi nchini wamekuwa wakipoteza maisha kutokana na sababu zinazoweza kuzuilika.

Awali, wakati akifungua mkutano huo, Kaimu Mwakilishi Mkazi wa UNFPA), Dk. Wilfred Ochani amaesema kuwa wao wataendelea kushirikiana na serikali katika kusaidia huduma za afya ya uzazi nchini.

“Kila mwaka UNFPA imeendelea kuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na TAMA kuhakikisha kuwa maadhimisho hayo yanafanyika kwa tija nakwamba kwa kusaidia wakunga kutaweza kuokoa maisha.

“Pamoja kwa kuwezesha wakunga tunaweza kuokoa maisha kwa ustawi wa Taifa letu, hivyo Waandishi wa habari mna mchango mkubwa katika kuokoa maisha ya akina mama kwa kutumia vyombo vyenu vya habari kufikisha ujumbe.

“Wakunga ni watu wanaopaswa kujeshimiwa sana na kuangaliwa kwa ukaribu kutokana na umuhimu wao kwa jamii kwani.

“Unfpa itaendelea kufanya kazi kwa kushirikiana na Serikali, imefanya ukarabati wa vituo vya afya na vifaa tiba katika mikoa ya Kigoma, Simiyu na Zanzibar, pia imeendelea kusaidia kutokomeza ukatili wa kijinsia katika mikoa ya Dodoma.

Felista Bwana kutoka Shirika la Umoja wa Taifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi (UNFPA)

“Ndio maana pia tunaboresha vituo vya afya hapa nchi ili kuokoa vifo kwa akina mama wanaopoyeza maisha wakati wa kujifungua na hii inefanyika katika mikoa ya Simiyu na Kigoma, ambapo itasaidia kuokoa maisha ya akina mama wanojifungulia njiani, pia kupata visa muhimu vinavyoweza kumsaidia mama wakati wa kujifungua,” amesema Dk. Ochani.

kwa mujibu wa Dk. Ochani hadi sasa UNFPA imesaidia nchi 120 duniani kote katika kuhakikisha kuwa inapunguza Vifo vya mama na mtoto.

TAMA ambayo ilianza ikiwa na wananchama 100 pekee hadi sasa ina jumla ya wanachama zaidi 4,000.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,719FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles