23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Takukuru yawaita wakulima waliodhulumiwa fedha za matrekta

Na MOHAMED HAMAD-MANYARA

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imewataka wakulima ambao fedha zao zilichukuliwa kwa udanganyifu kwa ahadi ya kununuliwa matrekta wawasilishe malalamiko yao ili waweze kurudishiwa fedha hizo.

Hatua hiyo inafuatia baada ya wakulima wawili kutoka wilayani Hanang’ mkoani Manyara kuilalamikia kampuni moja kwa madai ya kuchukua fedha zao na kushindwa kuwapatia matrekta hadi sasa.

Akizungumza na waandishi wa habari Mjini Babati jana, Mkuu wa Takukuru mkoani Manyara, Holle Joseph, alisema kampuni hiyo inapaswa kurejesha fedha hizo kabla ya Novemba 18 ili ziweze kurejeshwa kwa wakulima hao wa Wilaya ya Hanang’.

Kulingana na Takukuru, kampuni hiyo inatakiwa kurudisha Sh milioni 33.2 za wakulima hao ambapo mmoja alitoa Sh milioni 17 na mwingine Sh milioni 16.2 ili wanunuliwe matrekta lakini hadi sasa hawajapatiwa.

Makungu alisema mkurugenzi wa kampuni hiyo alipewa fedha hizo na wakulima hao ili awanunulie matrekta lakini ziliingizwa kwenye akaunti yake binafsi badala ya akaunti ya kampuni.

“Katika uchunguzi wetu tumebaini kuwa alielekeza fedha hizo kwenye akaunti yake binafsi badala ya kampuni jambo linaloashiria nia ovu na kwa sheria zilizopo anaweza kushtakiwa kwa makosa ya jinai yakiwemo ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu au kutakatisha fedha hizo.

“Rais Magufuli katika awamu yake ya pili ya uongozi wa nchi hii ameahidi atahakikisha rushwa na dhuluma zinatokomezwa na sisi tunatekeleza hilo kwa kufanyia kazi taarifa hii hata kama imetokea muda mrefu kwani jinai haifi hadi mtenda jinai atangulie mbele ya haki,” alisema Makungu.

Alimtaka mkurugenzi huyo awasilishe fedha hizo kwa mkuu wa Takukuru kabla ya Novemba 18 ili ziweze kurejeshwa kwa wakulima hao na kwamba kushindwa kutekeleza agizo hilo kutalazimisha kuchukua hatua zaidi kwa misingi ya sheria zinazotawala eneo hilo.

“Ni rai yetu iwapo kuna wakulima wengine ambao fedha zao zilichukuliwa kwa udanganyifu wa kuletewa matrekta na hawakuletewa wawasilishe malalamiko yao kupitia namba yetu ya dharura 113 au simu ya mkononi 0738 150 124 ili yashughulikiwe kwa pamoja,” alisema Makungu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles