24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Misongamano mijini kichocheo ongezeko ugonjwa wa kisukari

Na AVELINE KITOMARY -DAR ES SALAAM

INAKADIRIWA kuwa huenda ongeze-ko la ugonjwa wa kisukari likawa kub wa zaidi barani Afrika kutokana na kuongezeka kwa misongamano katika miji ya Bara ya hilo.

Hayo yalibainishwa jana na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Homoni katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Dk Wolfagang Bernard ikiwa ni kuelekea siku ya kisukari Duniani No- vemba 14 kila mwaka.

Dk Bernard ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani, alisema takribani miaka 30 iliyopita Dunia ilikuwa na wagonjwa wa kisukari mil-

ioni 30 lakini mpaka kufikia sasa, idadi ya wagonjwa inakadiriwa kuwa milioni 463, ambalo ni ongezeko kubwa ikilin- ganishwa na ongezeko la watu Duniani, ambapo awali walikuwa bilioni 4.5 na sasa ni bilioni 8.

“Sasa utaona ongezeko la watu Duniani ni mara mbili, lakini ongeze- ko la ugonjwa wa kisukari ni zaidi ya mara 150 huu ugonjwa wa kisukari unaongezeka kwa kasi sana na kasi hii ikiendelea makadirio yajayo ni kwamba mwaka 2030 yaani miaka 10 ijayo idadi ya ya watu wenye kisukari duniani itakuwa ni Milioni 600 na miaka 25 ijayo mwaka 2045 idadi ya wagonjwa itakuwa milioni 700.

“Kwa Afrika inakadiriwa ongezeko

litakuwa kubwa zaidi na sababu kub- wa ni mabadiliko ya maisha ya watu kwamba watu wanahamia Miji ambapo utaona katika miji ya Afrika mikusanyiko inakuwa kwa kasi sana.

“Sasa mtu anapohamia mjini kuna baadhi ya shughuli za mwili zinapun- gua ukubwa kwa Afrika sasa hivi ni mil- ioni 19 huku Tanzania ikiwa na wagojwa milioni 1.5, lakini sasa hawa ni wale wa- najulikana kwani wagonjwa wa kisukari hawaoneshi dalili sana,” alibainisha Dk Bernard.

Alisema hata hivyo huenda idadi ya wagonjwa wa kisukari ikawa kubwa zaidi kutokana na wagonjwa wengi ku- tokugundulika mapema.

“Watu wanaishi na ugonjwa wa

kisukari muda mrefu bila kujijua, hawa milioni 1.5 ni wale wanajulikana lakini huenda wasiojulikana wakawa wengi zaidi.

“Kwa hali hii kama hatutapeana taarifa na hatutachukua tahadhari ongezeko la kisukari Tanzania na Du- niani kwa ujumla linatisha,” alisisitiza.

Dk Bernaed alisema ugonjwa huo usipodhibitiwa unaleta madhara na inakuwa vigumu kutibika.

“Kwa kadiri sukari inavyoendelea inachoma viungo vya mwili, inapo- fusha macho, inaua figo, mishipa ya fahamu, mishipa ya damu, ganzi, vid- onda na moyo kushindwa kufanya kazi na hayo madhara ni makubwa sana hayawezi kurekebishwa.

Alisema endapo mtu antawahi anaweza kupatiwa matibabu ambayo yatadhibiti madhara hayo kwa kuweka kiwango sawa cha sukari mwilini.

“Ugonjwa huo dawa zake zimepa- tikana muda mrefu uliopita kwa wale ambapo kongosho imeharibika wa- nahitaji insulin hii ni sinadano ambayo anatakiwa mtu kuchomwa mara mbili au tatu kwa siku ili insulin imsaidie ku- pungza sukari kwenye damu,” alisema.

Daktari huyo alishauri njia ya ku- zuia ugonjwa huo kuwa ni mtindo bora wa maisha ikiwemo ulaji wa vyakula vinavyofaa na kufanya mazoezi.

“Njia ya kuzuia ni rahisi kufanya mabadiliko ya mtindo wa maisha kama kupunguza uzito, kufanya mazoezi, kuepuka kula vyakula vyenye sukari kwa wingi,kuepuka kunywa pombe, uvutaji wa sigara.

“Utumiaji wa sukari kwa win- gi kama kuongeza sukari kwenye chai,kunywa juisi yenye sukari na men- gine unachosha kongosho na itashind- wa kukusaidia.

“Tunashauriwa hasa katika waka- ti huu wa mabadiliko ya maisha ni muhimu kufanya mazoezi walau daki- ka 30 kwa siku,” alishauri Dk Bernard.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles