25.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 29, 2022

Contact us: [email protected]

Tatizo la kigugumizi na namna kivayotibiwa

Na AVELINE KITOMARY

KIGUGUMIZI ni hali inayomfanya mtu ashindwe kuongea vizuri, ambapo huongea kama anarudia maneno au anakwama katika maongezi yake.

Wataalamu wa afya wanasema hali hiyo ni ugonjwa unaoweza kumpata mtu kutokana na sababu tofauti tofauti.

Watoto wa kiume ndio wana- tajwa kuwa wanaathirika zaidi na ugonjwa wa kigugumizi kuliko wa kike kutokana na sababu za urithi wa haraka katika vinasaba.

Hata hivyo, katika jamii hali ya kigugumizi huwapata watu huku kukiwa hakuna ufahamu wa kutosha kuhusu ugonjwa huo na wakati mwingine kuchukuliwa kuwa hali ya kawaida.

Wakati mwingine ugonjwa huo wa kigugumizi huhusishwa na imani za kishirikina kama vile roho ovu kutajwa kumwingia mtu au mtoto.

Lakini pia, wapo wanaohisi kuwa ugonjwa huo unaweza kuwa tatizo la akili kitu ambacho sio kweli.

Ufahamu mdogo huleta imani za aina tofauti kwa jamii na hali hiyo hufanya watu wenye ugonjwa huo kuishi maisha yasi- yokuwa na furaha kwa kukosa kujiamini kuzungumza mbele za watu.

Rashid Majid (36), mkazi
wa Sinza, jijini Dar es Salaam, alizaliwa akiwa na kigugumizi lakini licha ya kuwa na hali hiyo hajawahi kufahamu kama huo ni ugonjwa unaohitajika kutibiwa.

“Tangu nikiwa mtoto nilikuwa na hii hali ya kigugumizi, sijawa- hi kupelekwa au kwenda hospi- tali kutokana na mimi mwenye kuiona hali hii ni ya kawaida hata watu walionizunguka wanaona ni kawaida.

“Kwahiyo, hata unavyoniam- bia ni ugonjwa nashangaa na sio mimi tu hata watu wengi hawa- jui kama ni ugonjwa,” anaeleza Rashid.

Mwandishi wa makala hii alipomuuliza kama ameweza kupata athari yoyote kwa hilo tatizo alijibu; “Kuna watu wengine wameshanizoea na wananichukulia kawaida, lakini kuna wale ambao nikikutana nao na kuzungumza nao wananishangaa, hii hunifanya kukosa ujasiri wakati ninapozungumza, inaathiri kiwango changu cha kujiamini,” anabainisha.

Maelezo ya Rashid yanaone- sha uhalisi wa uelewa mdogo wa jamii kuwa kigugumizi ni ugonjwa na unaweza kutibika. Lakini sasa, kuna haja ya jamii kufahamu hilo ili kuwasaidia wanaokumbwa na tatizo hilo.Ili kuendelea kutoa elimu
na matibabu ya ugonjwa huo, mwaka 2011 Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), iliamua kuanzisha kitengo maalum kwaajili ya kuhudumia watu we- nye ugonjwa wa kigugumizi.

“Kutokana na wingi wa mahi- taji unaoonekana katika vitengo mbalimbali, sasa tuna miaka tisa wagonjwa wameongezeka ndani na nje ya hospitali,” anasema Rukia Mohammed ambaye ni Mtaalamu wa Matamshi hospi- talini hapo.

ATHARI WANAZOPATA WAGONJWA WA KIGUGUMIZI

Rukia Mohammed anasema zipo athari ambazo mtu mwenye tatizo la kigugumizi anaweza kupata endapo kama hatapata matibabu yanayotakiwa.

Akizungumza na MTANZA- NIA katika mahojiano maalum jijini Dar es Salaam, Rukia anasema kutokana na athari hizo ni bora mgonjwa akapatiwa matibabu mapema ili kuweza kuepuka athari wanazopata.

“Athari wanazopata wagonjwa hawa ni kutumia nguvu nyingi wakati wanapozungumza, uhaba wa mwingiliano wa watu kutoka- na na hofu ya kuchekwa wakati wanapozungumza, hawaweze kuhuduria mikutano na kuongea, hayo yote huwafanya wajitenga.

“Hali hiyo huwafanya kukosa amani, wengine wanapata mson-

go wa mawazo, waoga kujitokeza, wanakosa nafasi katika sehemu mbalimbali, wanadharauliwa na kuchekwa,” anabainisha Rukia.

UNYANYAPAA UNAWAUMI ZA

Unyanyapaa unatajwa kuwa- kumba wagonjwa wenye kigu- gumiza, hii hutokea pale wana- potaka kujieleza na kushindwa au kutopewa nafasi mbalimbali kutokana na hali yao.

Rashid anasema kuwa wapo watu wenye tabia ya kutokum- sikiliza kutokana na kushindwa kuongea inavyotakiwa.

Anasema akifanya kosa anashindwa kujitetea kutokana na mkosoaji kuigiza sauti ya hali yake hiyo.

“Wakati mwingine naweza kukosa fursa kwa sababu ya hali yangu ya kigugumizi na wengine wakiona nashindwa kuongea hawanisikilizi tena hili linaniu- miza,” anaeleza kwa masikitiko.

Si kwake tu, mtaalam Rukia anasema wagonjwa wanaofika kupata matibabu pia wanaelezea kukumbwa na tatizo la unyanya- paa katika jamii.

Rukia anatoa ushauri kwa jamii kuacha kuwatenga na kuwanyanyapaa watu wenye ugonjwa huo na badala yake wawasaidie.

“Watu waelewe kuwa mtu ak- iwa na tatizo hapaswi kuchekwa bali asaidiwe na kupewa moyo pamoja na kumshauri aende hos- pitali kuliko kukaa naye nyum- bani,” anasisitiza.

AINA ZA KIGUGUMIZI

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Masikio, Pua na Koo, ku-
toka hospitali hiyo, Dk. Rachel Mkumbo, anasema kuwa aina za kigugumizi ziko mbili.

“Kuna ile inayoanza kwa mtoto kuanzia miaka miwili hadi sita wakati wa kujifunza kuongea

gea, ila tunategemea kigugumizi hicho kikaishia umri ambapo mtoto anaanza shule.

“Kuna watoto ambao katika umri huo kigugumizi kinaisha lakini kuna asilimia ndogo kama moja kigugumizi kinaendelea hadi utu uzima.

Dk. Mkumbo anabainisha kuwa aina ya pili ni ile inay- oanza baadae kwa watu wazima au kwa watoto haohao, hali hiyo huweza kutokea baada ya kupata ajali au kuumia kichwa au kupata kiharusi.

KUSHINDWA KUMTAZAMA MTU NI DALILI

Dk. Mkumbo anasema mo- jawapo ya dalili ya kigugumizi ni kushindwa kuanza au kumalizia maneno wakati wa kutamka.

“Zipo dalili za kigugumizi kama kushindwa kuongea wakati wa kutamka maneno mfano neno wewe anaanza ‘weeee- weeewewe’ au kupata shida ya kurefusha sauti mfano neno nak- wenda anasema ‘naaaaaaakwen- da,’ kurudia maneno na huwa kigugumizi kinakakuwa zaidi katika herufi za K na G mfano, neno kaka atasema ‘kaakakaka’ hizo ni moja ya herufi ambazo wanapata kigugumizi,” anasema Dk. Mkumbo.

Anataja dalili zingine kuwa ni kutafuta maneno na kushindwa kumtazama mtu usoni kutokana na hofu.

“Mtu mwenye kigugumizi anaweza kupata shida ya ma- cho kuchezacheza, kutetemeka midomo na kufunga mkono katika kuongea,” anafafanua Dk. Mkumbo.

Anashauri jamii kutoku- puuzia dalili hizo na badala yake wawapeleke watu wenye mata- tizo hayo hospitalini.

“Niwaambie jamii kuwa ugonjwa huu unatibika endapo mtu mwenye tatizo atapelekwa hospitali na kupatiwa matibabu, waachane na imani potofu kuhusu ugonjwa huu na waache kuwanyanyapaa watu wenye kigugumizi,” anashauri Dk. Mkumbo.

MATIBABU

Dk. Mkumbo anasema ugonjwa huo unatibiwa kwa njia mbili, ambazo ni tiba ya mazoezi na dawa.

Anasema matibabu huanza kutolewa endapo mtaalamu wa afya atamchunguza muhusika na kujua anahitaji kutibiwa aina gani.

“Lakini matibabu makubwa tunayoyaangalia ni yanayohusina na therapy (tiba shufwaa), suala la dawa halipo katika kutibu kigugumizi labda kama kunasa- babu zingine inayoleta kigugu- mizi.

“Matibabu ya kisaikojia; kum- fanya mtu ajitambu ajenge kuji- amini asiogope kuongea mbele za watu kujieleza na kujitambua.

“Tunatumia pia matibabu ya pumzi, kwani ili awaze kuongea vizuri inahitaji kwanza kifua chake kiwe kinakubali, anahitaji kuwa na pumzi ya kutosha ili aweze kutoa neno, tunawapa mazoezi, atavuta pumzi halafu atatoa taratibu, pia kuna mazoezi ya kusoma kwa sauti na kujieleza mbele za watu,” anaeleza Dk.Mkumbo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,444FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles