25.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 29, 2022

Contact us: [email protected]

Takukuru Mkoa wa Shinyanga yaokoa milioni 42/-

 SAM BAHARI

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Shinyanga katika kipindi Aprili hadi Juni 2020 imefanikiwa kuokoa Sh milioni 42 kati ya Sh milioni 110 za wazee watano wastaafu walioathirika na mikopo umiza.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu Takukuru Mkoa wa Shinyanga, Hussein Mussa alisema fedha hizo zilizookolewa kutoka kwa wakopeshaji mbalimbali zilikabidhiwa kwa wazee watano wastaafu kama walivyotapeliwa na wakopeshaji.

Mussa aliyataja makampuni hayo kuwa ni Malicha Microcredit Co Ltd, Nyakiha Co Ltd pamoja na watu binafsi ambao huendesha biashara ya kukopesha fedha kwa riba kubwa bila ya kuwa na leseni kinyume na sheria.

Licha ya kurejesha fedha hizo pia alisema katika kipindi cha robo ya nne ya mwaka wa fedha 2019/2020 Aprili hadi Juni 2020, Takukuru kupitia dawati la kuzuia rushwa imeendelea kufuatilia miradi miwili ya afya na elimu yenye thamani ya Sh milioni 411 iwapo itabainika kuwa na ubadhirifu sheria itachukua mkondo wake.

 Kwa mujibu wa Dawati la uchunguzi Takukuru kwa kipindi cha robo ya tatu Aprili hadi Juni cha mwaka wa fedha 2019/2020 zilipokelewa taarifa 76 ambazo baadhi uchunguzi umekamilika na nyingine bado unaendelea. 

Alisema kuwa idara zilizolalamikiwa ni pamoja na mikopo umiza (12), serikali za mitaa (12), ushirika (8), elimu (6), Taasisi za fedha(6), Afya (5), Mahakama (5), Ardhi (5), siasa (4), polisi (4), ujenzi, (3) madini (2), kilimo (2) na maji (2).

Kesi zinazoendelea mahakamani ni 30 kati ya hizo kesi mpya ni tano na kesi mbili ziliamuliwa mahakamani kwa watuhumiwa kutiwa hatiani kwa kushitakiwa kulipa faini.

Mchanganuo wa kesi zinazoendelea mahakamani kisekta ni pamoja na Serikali za mitaa (13), elimu kesi (7), idara ya afya (3), uhamiaji (1), Nida (1), usafirishaji (1), Tasaf (1), michezo (1) Taasisi za fedha (1) na mahakama (1).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,454FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles