23 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

TACAIDS, UN WOMEN wawanoa wanahabari kuhusu maambukizi ya VVU na Jinsia

Na Faraja Masinde, Mtanzania Digital

Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) imesema vyombo vya habari ni nguzo muhimu katika kufikisha ujumbe kwa jamii juu ya masuala ya virusi vya Ukimwi na jinsi ya kundoa unyanyapaa ambao umekuwa ni kikwazo.

Sehemu ya Wahiriki wa Warsha hiyo.

Akizungumza mara baada ya warsha ya siku mbili ya kuwajengea uwezo wanahabari kutoka vyombo mbalimbali iliyofanyika mjini Bagamoyo, Afisa Jinsia kutoka Tacaids, Judith Luande, amesema lengo ni kuona wananchi wanapata habari sahihi zinazohusu masuala ya Ukimwi.

“Vyombo vya habari ni nguzo muhimu katika kutoa habari sahihi zinazohusiana masuala ya Ukimwi kwa mtamzamo wa kijinsia na kuona ni jinsi gani tunaweza kutumia vyombo vya habari ili kuweza kufikisha ujumbe kwa wananchi kuhusiana na masula ya VVU na Ukimwi na kuondoa vikwazo hivyo.

“Hivyo, tunaamini kuwa kutokana na umuhimu wa wanahabari katika jamii na mafunzo haya waliyoyapata basi watasaidia kuweza kufikisha elimu hii,” amesema Judith.

Awali, Mratibu wa Programu za Ukimwi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uwezeshaji wa masuala ya Wanawake (UN Women), Jacob Kayombo, amesema kundi la wanahabari ni muhimu katika kudhibiti ukimwi na masuala ya jinsia na kwamba iwapo watashirikishwa vizuri watatoa mchango mkubwa.

“Tumegundua kwamba wanahabari ni watu muhimu katika kudhibiti ukimwi na masuala ya jinsia ikiwamo kuondoa unyanyapaa. Hivyo kama tutawashiriki vizuri wananhabari katika mapambano dhidi ya Ukimwi basi tutakuwa tumeisaidia jamii kupata uelewa mkubwa na kuwa na mtazamo chanya kuhusu ukwimwi,” amesema Kayombo.

Akizungumzia mafunzo hayo mmoja wa washiriki, Jacob Sonyo kutoka Morogoro, amesema yamemsaidia kuongeza ufahamu kuhusu VVU na Ukimwi.

“Mafunzo haya yamekuwa na msaada mkubwa kwangu kwani yamekuja kipindi muafaka ambapo tunashuhudia hali ya unyanyapaa kwenye maeneo mbalimbali nchini, hivyo nawashukuru Tacaids na UN WOMEN kwa kutujengea uwezo huu,” amesema Sonyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,250FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles