23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 8, 2023

Contact us: [email protected]

Tabora waahidi kuishangili Biashara United

Na Shomari Binda, Tabora

Mashabiki na Wapenzi wa soka mkoani Tabora, wameahidi kuishangilia timu ya Biashara United kwenye mchezo wake utakaopigwa kesho Ijumaa Juni 25, 2021 dhidi ya Yanga.

Mchezo huo ni wa hatua ya Nusu Fainali wa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) ambao utakutanisha vigogo wa soka nchini Yanga na Wanajeshi wa mpakani Biashara United.

Wakizungumza na MtanzaniaDigital Alhamisi Juni 24, 2021 kwa nyakati tofauti mkoani Tabora, mashabiki hao wamesema wapo tayari kuiunga mkono timu hiyo.

Wamesema timu ya Biashara United ipo salama mkoani humo na wataishangilia kwa nguvu ili kuwapa nguvu.

Mmoja wa mashabiki hao aliyejitambulisha kwa jina la Mussa John mkazi wa Uyuhi amesema Biashara United ni timu bora na itashinda dhidi ya Yanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,353FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles