23.2 C
Dar es Salaam
Friday, June 9, 2023

Contact us: [email protected]

Shindano la Miss Ilala lazinduliwa

Na Brighter Masaki, Dar es Salaam

Muandaaji wa shindano la Urembo la Miss Ilala wamesema fainali ya kumpata mlimbwende atakayepeperusha bendera ya wilaya hiyo itafanyika Julai 31, 2021.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam katika hafla ya uzinduzi wa shindano hilo iliyofanyika Juni 23, mwaka huu.

Mwandaaji wa shindano hilo, Lucas Rutainiwa amesema shindano hilo limeanza  rasmi na kwamba tayari usaili wa washiriki umekamilika.

“Leo tumezindua shindano la Miss Ilala ambalo fainali yake itakuwa Julai 31. Hivyo warembo watakuwa wanakuja mazoezini na kurudi nyumbani, hawatakaa kambini hadi siku ya failani na baada ya hapo washindi watatu wataenda kuwakilisha ngazi ya Miss Tanzania.

“Washindi hao watakutana na warembo wa Tanzania nzima wakiwemo na wamikoani na kupatikana mrembo mmoja atakae wakilisha Tanzania kimataifa kwenye shindano la mrembo wa dunia (Miss World),” amesema Rutainiwa.

Aidha, pia amemshukuru Rais Samia Suluhu, kwa kumteua Muandaaji wa Shindano la Miss Tanzania, Basila Mwanukuzi na kumpongeza kwa kuaminiwa na kupewa nafasi hiyo ya heshima.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,351FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles