25.3 C
Dar es Salaam
Friday, May 3, 2024

Contact us: [email protected]

Taasisi, wadau watakiwa kushirikiana kumlinda mlaji

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji amewataka washiriki wa kongamano la kilele cha maadhimisho ya Haki ya Mlaji Duniani kujadiliana kwa kina kutafuta ufumbuzi wa pamoja wa changamoto zinazoletwa na ukuaji wa sayansi na teknolojia katika kusambaza bidhaa na huduma na jinsi ya kumlinda mlaji.

Akisoma hotuba kwa niaba ya waziri huyo, leo Machi 15,2024, jijini Dar es Salaam , Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk Hashil Abdallah katika kongamano lililoandaliwa na wakati Tume ya Ushindani Nchini (FCC), amesema ni muhimu kuimarisha matumizi ya mifumo ya teknolojia katika utendaji wa taasisi za umma.

“Ili kujadili dhana ya akili mnemba na jinsi gani mlaji anapaswa kulindwa dhidi ya changamoto mbalimbali zinaweza kusababishwa na teknolojia hiyo, jambo hili ni la kupongezwa kwa kuwa dunia ndiko inakoelekea na Tanzania inabidi kuwa tayari kukabiliana na teknolojia hiyo kwa kuwa nchi yetu si kisima,”amesema.

Amesema matumizi ya akili mnemba katika utoaji huduma kwa walaji ni dhana mpya ambayo kwa sasa imeshika kasi duniani kote.

Ameeleza kuwa ni eneo linalokua kwa kasi hivyo ni jambo muhimu kwa vyombo usimamizi wa uchumi wa soko vinavyotoa huduma kwa wananchi kama FCC pamoja na taasisi nyingine zinazoshughulika na biashara kuimarisha matumizi ya mifumo.

“Kulingana na uzoefu wa kimataifa kama ilivyoelezwa na taasisi huru ya kutetea walaji duniani ili kuwezesha kupatikana kwa udhibiti na uhakika wa matumizi ya akili mnemba katika kutoa huduma kwa walaji unazingatia uwajibikaji na maslai yao kwa ujumla,” amesema.

Amefafanua kuwa mifumo hiyo kwa kiasi kikubwa huhitaji taarifa nyingi katika kufanikisha uundwaji na utendaji wake, hivyo wanapaswa kuhoji na kutafiti namna ambavyo mifumo hiyo inavyoundwa na kusimamiwa na endapo hayo yatafanyika kwa kulinda maslahi ya mlaji ni dhahiri itasaidia kufikia malengo.

Aidha amebainisha faida na athari zake katika huduma za mlaji ili kuwezesha kutunga sera, Sheria mifumo ya usimamizi na udhibiti pamoja na watafiti.

Ameongeza kuwa serikali kupitia mamlaka zake wataendelea kuweka utaratibu wa kudhibiti utakao wataka watoa huduma wana tumia mifumo ya teknolojia hizo kuweka bayana changamoto zinazoweza kujitokeza kwa walaji na kutumia teknolojia hiyo kuelimisha jamii ili kuwa makini wanapotumia.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa FCC, William Erio amesema ni ahadi ya baraza kuendelea kushirikiana na mamlaka za udhibiti pamoja na FCC katika kuhakikisha kwamba wanaendeleza sheria za ushindani, udhibiti na kumlinda mteja.

Amesema lengo kubwa la sheria za ushindani sio tu kuwalinda washindani bali kumlinda mlaji, hivyo pale wanapoona sheria hizo zinashindwa kumlinda mlaji ipasavyo wanayo fursa kuzibadilisha ili kuendana na hali ambayo ipo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Tanzania( CTI ), Mhandisi Leodger Tenga amesema elimu waliyotoka nayo kwenye mkutano huo watakwenda kuwashirikisha wenye viwanda kwani kuna mengi mapya wameyaona.

Kwa upande wake Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk. Eliezer Feleshi amesema kuna umuhimu wa kuhakikisha kunakuwepo na sheria ambazo zitawaleta katika ulimwengu sawa ndani ya Tanzania.

Amesema inahitajika bajeti ya kutosha kuwezesha FCC na ZFCC kufanya shughuli zake kwa urahisi kwani maeneo ya walaji haki zao zinaendana na tafiti na matokeo ya kila siku.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles