TAASISI BINAFSI ZATAKIWA KUJISAJILI SERIKALINI

0
446
Mkurugenzi Mkuu TCDD, Hebron Mwakagenda

 

Na FERDNANDA MBAMILA, DAR ES SALAAM

MTANDAO wa Madeni na Maendeleo Tanzania (TCDD), umezitaka taasisi na mashirika binafsi kujisajili serikalini ili kuondoa mkanganyiko wa uhalali wa taasisi zao utakaojitokeza.

Akizungumza Dar es Salaam juzi katika warsha iliyoshirikisha wadau wa taasisi na asasi mbalimbali nchini, Mkurugenzi Mkuu TCDD, Hebron Mwakagenda, alisema kabla ya taasisi kuanza kufanya kazi na kujulikana, ni lazima isajiliwe na kukaguliwa ili ziweze kufanya kazi kwa uhuru na Serikali pamoja na mashirika binafsi.

“Ili taasisi isajiliwe na kujulikana na Serikali, ni lazima kufuata kanuni taratibu na masharti, lengo ni kupata hesabu halisi ya mashirika na taasisi zinazo tambulika na serikali.

“Hadi sasa TCDD ina zaidi ya mashirika na taasisi 800 binafsi  nchini, ambayo zimesajiliwa na kutambulika na Serikali,” alisema Mwakagenda.

Alisema wanawasisitiza watu kujisajili baada ya kuona baadhi ya mashirika na taasisi binafsi zinaanza kufanya kazi zinazokiuka maadili katika jamii.

“Endapo taasisi zitasajiliwa na kujulikana na Serikali itakuwa imekidhi vigezo na kutii maagizo ya kanuni na taratibu za usajili,” alisema.

Alisema TCDD hufanya usajili kila mwaka na kutoa taarifa kwa taasisi husika, ili kuwajulisha wadau mabadiliko yaliyojitokeza na kuyafanyia kazi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here