25.1 C
Dar es Salaam
Saturday, October 23, 2021

Sven aifungia kazi Yanga, hapatoshi J’pili

 WINFRIDA MTOI -DAR ES SALAAM 

KUELEKEA mechi na watani zao Yanga, Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, amesema leo anaanza rasmi kuandaa silaha za kuwakabili mahasimu wao, Yanga katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC). 

Mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na wapenzi wa soka hapa nchini na kwingineko, utachezwa Jumapili hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 

Wanamsimbazi hao walitua jijini jana asubuhi wakitokea Mtwara baada ya kucheza michezo miwili ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Ndanda FC na Namungo FC, kisha kukabidhiwa kombe la ubingwa wa msimu huu. 

Akizungumza na MTANZANIA jana, Sven alisema muda wote alikuwa haiwazi Yanga, alikifahamu maandalizi yake yatafanyika Dar es Salaam. 

Alisema mchezo huo ni mkubwa na mgumu, unaohitaji mipango na mbinu kuhakikisha ushindi unapatikana, hivyo leo anaanza mazoezi rasmi kwenye Uwanja wa Mo Simba Arena, uliopo Bunju, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya Yanga. 

“Tutajiandaa vizuri kwa uwezo wetu, kuikabili Yanga Jumapili, ilikuwa ni mipango yangu kuwa tukifika Dar es Salaam ndiyo tunaanza maandalizi katika uwanja wetu,” alisema Sven. 

Wakati huo huo, kikosi cha Wekundu wa Msimbazi hao jana kilipata mapokezi ya nguvu kilipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam, kwa mashabiki kujitokeza kwa wingi. 

Msafara huo ulikuwa na pikipiki na magari ya mashabiki, ulikwenda moja kwa moja kambini kwao, Mbweni, jijini baada ya Sven kugoma timu hiyo kupitia Makao Makuu yao yaliyopo Msimbazi kama ilivyokuwa imepangwa.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,953FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles