23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

SuperSport yaitaka Ligi Kuu Bara

NA SELEMAN SHINENI, MAURITIUS

KAMPUNI ya MultiChoice Africa kupitia channel zake za SuperSport, inatarajia kuonyesha michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), baada ya mkataba wa Azam kuonyesha ligi hiyo kufika tamati.

Azam waliingia mkataba wa kuonyesha ligi hiyo mwaka 2014, ambapo mkataba huo unatarajiwa kumalizika katika msimu wa 2017.

Akizungumza na MTANZANIA jana, wakati wa tamasha la 2015 Content Showcase Extravaganza, Mkurugenzi wa SuperSport Kusini mwa Afrika, Graeme Murray, alisema wamejipanga kununua haki za kuonyesha VPL baada ya Azam kumaliza mkataba wao.

“Baada ya mkataba wa Azam kwisha tuna mpango wa kurudi kujaribu kununua tena haki za televisheni za Ligi Kuu Tanzania Bara,” alisema Murray.

Murray alieleza wakati wanasubiri suala hilo lifanyike, wataendelea  kuonyesha michuano mbalimbali ya Baraza la Michezo Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).

Hata hivyo, alisema kabla ya Azam kuanza kuonyesha ligi, wao walikuwa na mpango wa kununua haki za televisheni za ligi hiyo, lakini hawakuwa na jinsi zaidi ya kukaa pembeni kuwapisha.

“Sababu za kuamua kurudi tena kutaka kununua haki za televisheni za VPL zinatokana na maombi ya watazamaji wengi ambao wanahitaji kuona ligi hiyo,” alisema.

Akizungumzia michuano mbalimbali inayoonyeshwa kwenye SuperSport, Murray aliweka wazi kuwa chaneli zake karibuni zimesaini mkataba wa kuonyesha Ligi Kuu England kwa misimu mingine mitatu.

“SuperSport sasa iko kwenye mchakato wa kufundisha watu kutoka mataifa mbalimbali jinsi ya kuonyesha soka katika ubora wa hali ya juu,” alisema.

Kampuni ya MultiChoice imefanya tamasha la wiki nzima katika visiwa vya Mauritius, ikiwa na lengo la kuonyesha jinsi walivyojipanga kuongeza ubora katika televisheni zao kwa mwaka ujao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles