23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Sunday Oliseh atoka kapa kwa Mkwasa

Sunday-OlisehNA BADI MCHOLO, DAR ES SALAAM

KOCHA wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa, anawaumiza vichwa wapinzani wake, timu ya Nigeria ‘Super Eagles’ baada ya kupata ugumu wa kushindwa kuelewa falsafa ya kocha huyo mzawa, badala yake wamebaki kutumia muda mwingi kuangalia video za michezo ya zamani.

Kocha wa Nigeria, Sunday Oliseh, licha ya kuwa katika nafasi nzuri ya pili katika kundi G linaloundwa na timu za Misri, Chad na Taifa Stars, amekuwa akikesha kuangalia video za Stars na kuvutiwa jinsi ilivyocheza michezo iliyopita.

Mtandao wa Supersport.com, umeeleza licha ya Oliseh kupata nafasi ya kuwaona Stars katika video, amekuwa bize kuwasoma, lakini ameendelea kuwa gizani kwa kutokujua nini Taifa Stars watafanya katika mechi hiyo Jumamosi.

“Naijua baadhi ya mifumo ya Stars kabla haijachukuliwa na kocha huyo mpya, nakiri kuwa na wakati mgumu kwa sasa.

“Tanzania tunaijua kuwa ina timu bora, lakini tunaamini tutakuja kushangazwa katika mchezo kutokana na kutojua mifumo ya kocha wao mpya, Mkwasa, kingine ambacho kitawasaidia Stars ni kuwa wako nyumbani,” alisema Oliseh.

 

Kutokana na hali hiyo ya sintofahamu kwa Nigeria, Shirikisho la soka nchini humo liliamua kutuma watu wake Tanzania kwa ajili ya kutafuta video za Stars ikinolewa na Mkwasa, lakini wameshindwa kuzipata mpaka timu hiyo ilipowasili jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo wa kuwania kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2017 (AFCON), unatarajiwa kupigwa kesho katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, mtandao huo ulieleza Oliseh amesema ana nafasi kubwa ya kushinda, licha ya mlinda mlango wake namba moja, Vincent Enyeama, kuachwa katika kikosi hicho.

“Nafasi ya Enyeama itachukuliwa na Carl Ikeme, ninaamini tutafanya vizuri kwa kuwa ana uwezo mkubwa, kumkosa Enyeama haimaanishi kuwa tutaupoteza mchezo huo, ninaamini tutafanya vizuri,” aliongeza Oliseh.

Mlinda mlango huyo tegemeo kwa sasa, Ikeme, amesema kuwa atahakikisha anaonesha uwezo wake katika mchezo huo kwa ajili ya kulitetea taifa lake.

“Nitahakikisha najituma kama ninavyo fanya nikiwa katika klabu yangu ya Wolverhampton Wanderers F.C. ya nchini Uingereza na kuonesha kiwango cha hali ya juu,” alisema Ikeme.

Kwa upande wake, kocha wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, Boniface Mkwasa, alisema alishaifahamu mikakati ya kocha huyo ambapo wamekuwa wakisaka kwa udi na uvumba kufahamu mfumo na falsafa anayotumia lakini hawajaufahamu hadi sasa.

“Ndio maana sitaki kuelezea mfumo ninaoutumia, utafahamika uwanjani, kwani taarifa zao za kuichunguza timu yangu kwa muda mrefu nimezipata,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles