27 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Sanjay Dutt aifagilia Tanzania


Na Mwandishi Wetu

MKALI wa filamu za kihidhi Boll, Sanjay Dutt amesema hakuna sehemu bora duniani kama Tanzania ambayo unaweza kutembelea na kuwekeza.

Sanjay Dutt ambaye ametamba na filamu mbalimbali tangu miaka ya 80 na kuchukua tuzo tofauti, yupo nchini tangu juzi Novemba 6,2021 na amekutana na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa.

Akizungumza baada ya kuwasili nchini, amesema siku zote amekuwa akimuambia kila mtu kuwa hakuna sehemu bora na nzuri kama Tanzania.

“Tanzania ni kama nyumbani kwangu, nimekuwa nikimuambia kila mtu nchini kwangu na hata Marekani na Uingereza kuwa hakuna sehemu bora duniani kama Tanzania, unaweza kuja kutembea, pia unaweza kuwekeza,” amesema Sanjay Dutt.

Sunjay Dutt enzi hizo

Kwa upande wake Waziri Bashungwa amesema watahakikisha ujio wa msanii huyo hapa nchini unakuwa na manufaa, huku akimuomba kushiriki sehemu ya filamu na wasanii wa Tanzania ili kuipa sapoti sanaa hapa nchini.

“Ujio wake hapa nchini unakuwa na manufaa kwenye malengo yake lakini pia na sisi kama nchi, tasnia ya filamu tunanufaika na ujio wake, haya ndiyo malengo ya Serikali.

“Umaarufu wake unaweza kuwasaidia wasanii wetu hapa nchini, kwa mfano yeye akicheza hata dakika tano kwenye filamu zetu, tumekuwa tumeshauza,” ameeleza Bashungwa.

Sanjay Dutt atatembelea maeneo mbalimbali ya kitalii ikiwamo Zanzibar, hii si mara ya kwanza msanii huyo kutembelea Tanzania mara ya mwisho ilikuwa 2017.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles