26.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 26, 2023

Contact us: [email protected]

Sugu aitaka Serikali kupunguza tozo hotelini

Ramadhan Hassan, Dodoma

Mbunge wa Mbeya Mjini,Joseph Mbilinyi (Chadema) maarufu Sugu ameitaka Serikali kupunguza tozo kwenye Hotel kwani zimekuwa zikiwarudisha nyuma wafanyabiashara.

Mbilinyi ametoa kauli hiyo leo Mei 24 bungeni wakati akichangia Mjadala wa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka 2019-2020.

Mbilinyi amesema tozo zinazotozwa kwenye hotel nchini zimekuwa nyingi hivyo ameiomba Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii iziondoe ili wafanyabishara wenye biashara zao ziweze kukuwa.

“Kuhusu Tozo zimekuwa nyingi, umekaa tu mara wanapiga hodi anasema anatoka sehemu fulani,amefuata tozo, hotel mpya mzipe miaka miwili bila tozo ili wakuze biashara zao.Niiombe Serikali itoe hizo tozo zimejaa sana ndio maana biashara hazikuwi,”amesema Mbilinyi.

Pia ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kutangaza utalii wa Ukanda wa Kusini.

“Waziri niambie kati ya watalii 1.5 milioni waliotembelea Tanzania ni wangapi wameenda kutembelea Ukanda wa Kusini,”amesema.

Mbilinyi amemtaka Waziri wa Wizara hiyo,Dk.Hamisi Kigwangala kwenda kujifunza vivutio vilivyopo nje ya Tanzania.

“Nenda Mamtoni katalii kaangalie watu wana fanya nini kaka utoke uende Ulaya ukajue watalii wanataka nini na sio ile chanel ya TBC badala ya kuonesha watalii wanaonesha miradi iliyofanywa na Tanapa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,726FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles