27.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 17, 2024

Contact us: [email protected]

Straika wa Chelsea atua Yanga

Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Seleman Abdallah Mbaruku, akiwa katika mazoezi ya timu ya Yanga jana kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari ya Loyola, Dar es Salaam. Picha na John Dande
Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Seleman Abdallah Mbaruku, akiwa katika mazoezi ya timu ya Yanga jana kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari ya Loyola, Dar es Salaam. Picha na John Dande

Na Abducado Emmanuel, Dar es Salaam

MSHAMBULIAJI wa zamani wa timu ya Chelsea ya England, Seleman Abdallah Mbaruku, ametua jana ndani ya kikosi cha Yanga kufanya majaribio ili kusajiliwa na timu hiyo.

Mbaruku amewahi kuichezea timu ya watoto ya Chelsea alipokuwa na umri wa miaka saba na nane, kabla ya kuhamia timu ya Coventry City inayoshiriki Ligi Daraja la Tatu nchini England, ambapo alicheza kwa miaka tisa kuanzia akiwa na miaka 10 hadi 19, timu hiyo iliwahi kucheza Ligi Kuu kwa misimu 34 kabla ya kushuka daraja mwaka 2001.

Akizungumza na MTANZANIA jana jijini Dar es Salaam, Mbaruku alisema amekuja kusaka nafasi ya kusajiliwa Yanga, pamoja na timu nyingine za hapa Tanzania zitakazoonesha nia ya kumsajili.

“Nimeletwa Yanga na Kampuni ya Afri Soccer ya Zanzibar, kwa ajili ya majaribio sio hapa tu pia nitafanya majaribio kwenye timu nyingine za hapa nitakazopangiwa na kampuni hiyo,” alisema Mbaruku.

Mbaruku, 22 na ameonekana kupata shida kwenye mazoezi ya jana asubuhi yaliyofanyika katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Loyola, uliopo Mabibo, jijini Dar es Salaam kutokana na umbo lake kubwa lakini amedai aliongezeka uzito baada ya kupata majeraha ya mgongo yaliyomweka nje ya dimba kwa miezi sita.

“Niliumia mgongo hivyo nililazimika kukaa nje ya dimba kwa miezi sita, hivi sasa ndio nimerejea uwanjani na nimekuja kusaka nafasi Yanga,” alisema.

Jaja apikwa mabao

Kwenye mazoezi ya jana kocha msaidizi wa Yanga, Leonardo Neiva, alianza kumpika mshambuliaji mpya wa timu hiyo raia wa Brazil, Geilson Santos Santana ‘Jaja’, namna ya kufunga mabao kuanzia mipira ya juu ya vichwa na miguu.

Neiva alitumia takribani dakika 15 kumpika Jaja, ambapo alimudu mazoezi hayo huku akipiga vichwa vya nguvu pamoja na mabao ya miguu, lakini Jaja alionekana kuchoka ndani ya muda wa programu hiyo.

Wakati Jaja akipiga tizi hilo, wachezaji wenzake walikuwa wakinolewa na kocha mkuu, Marcio Maximo, namna ya kupanga mashambulizi ya haraka haraka pamoja na ufundi kupitia mifumo ya 4-4-2, wakiwa wanashambuliwa na wapinzani na 3-5-2 wanapokuwa wanashambulia.

Mara baada ya mazoezi hayo, Neiva alisema hiyo si programu ya Jaja peke yake, bali wataendelea kuimarisha makali ya nafasi ya ushambuliaji kwa wachezaji wote wa nafasi hiyo.

“Nimeanza na Jaja tu, lakini programu kama hii pia watafanya wachezaji wengine wa nafasi hiyo kama Jerrson Tegete, Said Bahanuzi na Hussein Javu,” alisema Neiva.

- Advertisement -

Related Articles

2 COMMENTS

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles