27.5 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Ivo amfunika Casillas Simba

Kipa wa Simba, Ivo Mapunda
Kipa wa Simba, Ivo Mapunda

NA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM

MAKIPA wa timu ya Simba, Ivo Mapunda na Hussein Shariff ‘Casillas’, juzi wameoneshana umwamba wa kupangua mashuti yaliyokuwa yakipigwa na wachezaji wengine wa timu hiyo, huku Ivo akimfunika Casillas.

Makipa hao wanaoneshana umwamba ili kila mmoja kuipata nafasi ya kuwa kipa namba moja kwenye kikosi cha kocha, Zdravko Logarusic ‘Loga’raia wa Croatia aliyesaini mkataba wa mwaka mmoja Jumanne iliyopita.

Ivo alimfunika kipa huyo baada ya kuiongoza timu aliyokuwa akichezea yeye kuifunga timu ya Casillas mabao 4-2.

Mbwembwe hizo walifanya katika mazoezi ya Simba, yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), chini ya Loga na msaidizi wake, Selemani Matola.

Katika mazoezi hayo yaliyoanza majira ya saa 10 jioni, wachezaji walianza na zoezi la kupigana chenga kabla ya kuanza kukimbia kwa kuzunguka uwanja huo mara saba na kisha kuanza kuoneshana umwamba uwanjani.

Loga aliwagawa wachezaji kwenye makundi mawili na kutokana na upungufu wa wachezaji, ilibidi Matola ajiunge na timu moja iliyokuwa ikidakiwa na kipa Casillas, huku Meneja wa timu, Nicodemus Nyagawa, akijiunga na timu aliyokuwa akidaka Ivo.

Zoezi hilo lilikuwa la nusu uwanja, Ivo alionekana yupo makini katika kupangua mipira huku akiruhusu mabao mawili pekee kutikisa nyavu zake kutoka kwa wachezaji, Abdalah Sesseme na Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Casillas aliruhusu mabao manne yaliyofungwa na Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, beki Joseph Owino aliyefunga mawili na jingine lilifungwa na Uhuru Selemani.

Loga alizidi kuwapa mbinu wachezaji wake baada ya kuwafundisha namna ya kupiga penalti kiufundi, wachezaji wengi walilipatia zoezi hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles