24.8 C
Dar es Salaam
Sunday, April 28, 2024

Contact us: [email protected]

Startimes yazindua msimu wa pili wa Bingwa

Na Beatrice Kaiza, Mtanzania Digital

SHINDANO la Bingwa msimu wa pili limezinduliwa rasmi na kutambulisha washiriki zaidi ya 20 ikiwemo wale ambao wanafahamika kupitia mitandao ya kijamii.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 18, 2023 jijini Dar es Salaam, Meneja Mradi wa shindano hilo, Ombeni Phiri amesema kipindi cha Bingwa ni zaidi ya burudani ambapo msimu wa kwanza waliingia washiriki 18 ambao wengi wao ni vijana wenye ushawishi mkubwa kwenye mitandao ya kijamii na mmoja wao aliibuka mshindi na gari aina ya crown pamoja na pesa.

“Vijana ambao wanafahamika kupitia mitandao ya kijamii na watu maarufu wenye ushawishi mkubwa katika jamii hasa kwa watakuwepo ndani ya Bingwa ambapo kipindi hicho kitakuwa moja kwa moja kwenye chaneli ya TV3 inapatikana katika kisimbuzi cha StarTimes,” amesema Phiri.

Hata hivyo, ameeleza lengo la kuwepo kwa shindano hilo ni kuwapa fursa vijana Kujifunza vitu mbalimbali ikiwemo fursa zilizopo katika mitandao ya kijamii katika kukuza na kutengeneza brand zao.

Aidha, kwa upande wake Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes, David Malisa ameeleza kuwa kupitia msimu wa kwanza walipokea maoni mbalimbali kutoka kwa watazamaji namna ambavyo wangependa msimu ujao uboreshwe kwa baadhi ya vitu na ndio sababu iliyopelekea mwaka 2022 kusiwepo kwa shindano hilo.

Pia amesema shindano hilo ni daraja la kufunguka kwa fursa nyingi kwani hata usipofanikiwa kushinda unaweza kupata fursa ya kuwa balozi wa kampuni.

“Harmorapa alikuwa miongoni mwa washiriki kwa msimu uliopita, hivyo kampuni ya Startimes iliweza kumpa ubalozi wa mwaka mmoja ambapo fursa ya ushiriki wake ilianzia hapo kuonekana hakutoka mtupu pamojana washiriki wengine walipata kifuta jasho chao.

Pia, Malisa amewaambia watazamaji wa bingwa kulipia visimbuzi vyao kwani msimu wa pili una maudhui tofauti tofauti yenye kufunza ambapo hata watazamaji watapata elimu mbalimbali. 

Naye, Mshindi wa Bingwa msimu wa kwanza, Noel maarufu kama “Photogenic mtoto” amewaasa washiriki hao kuwa na nidhamu na kuendana na kauli mbiu ya shindano hilo isemayo “Najiamini kinoma” hivyo washiriki wanatakiwa kujiamini na kutumia fursa hiyo kutengeneza brand zao.

Hata hivyo, Photogenic amewatia moyo washiriki hao wanapoianza safari yao ya mafanikio wawapo katika shindano hilo ambapo ingizo jipya la washiriki msimu huu wa pili kuna sura mbalimbali zenye ushawishi katika  mitandao ya kijamii akiwemo Mchekeshaji, Mkali wenu, Amirado pamoja na Mwanamitindo Hamid .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles