23.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 27, 2024

Contact us: [email protected]

UDOM yawakaribisha wananchi maonyesho ya TCU Mnazi mmoja

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Watanzania mbalimbali wametakiwa kutembelea banda la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) lililopo katika Maonesho ya 18 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia mwaka 2023 kwa ajili ya kujifunza na kujiunga na programu mbalimbali za chuo hicho ikiwamo huduma za elimu na ushauri ambao unatolewa bure.

Dk. Ikunda Dionis Mushi, wa Shule ya Tiba na Kinywa, akitoa maelezo kwa washiriki wa maonesho, walipotembelea Banda ya UDOM.

Ikumbukwe kuwa maonesho hayo yanaratibiwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) yanaendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam yakiwa na kaulimbiu ya “Kukuza ujuzi nchini kupitia Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia, kwa Uchumi Imara na Shindani” yakishirikisha vyuo mbalimbali vya elimu ya juu nchini.

Akizungumzia maonyesho hayo leo Julai 18, 2023, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa UDOM, Rose Joseph, amesema banda hio linatoa elimu na ushari mbalimbali kwa wazazi na wanafunzi wanaotajiwa kujiunga na elimu ya juu ya juu.

Kwa mujibu wa Rose, Wataalam mbalimbali wa chuo hicho wapo kwa ajili ya kutoa huduma.

“Tunawakaribisha Watanzania katika banda letu la Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM) sababu hpa tunawataalamu wa kila fani ambao wanashiriki ili kutoa maelezo ya kina kwa wananchi wanaotembelea hapa,” amesema Rose.

Wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Dodoma wakiwahudumia wananchi waliofika kwa wingi kwenye banda lao, kupata maelezo ya programu na taratibu za udahili kwa Mwaka wa Masomo 2023/2024

Rose amezitaja baadhi ya huduma nyingine muhimu zinazotolewa kwenye banda hilo kuwa ni udahili wa moja kwa moja wa wanafunzi wanaotaka kujiunga na Chuo hicho kwa Programu mbalimbali za masomo kwa mwaka 2023/24, ushauri wa kitaalamu kuhusu programu, huduma za malazi na masuala mengine yanayohusu shughuli za Chuo Kikuu cha Dodoma.

“Kwa sasa Chuo Kikuu Dodoma kinatoa mafunzo katika fani za Udaktari, Uchumi, Sheria, Sosholojia, Utawala wa Biashara, Biashara na Uhasibu, Biashara katika Utawala na Rasilimali Watu, ujasiriamali, Biashara ya Kimataifa, Utalii, Masoko, Mazingira, Takwimu, Ununuzi na Ugavi, Mawasiliano na Teknolojia (TEHAMA).

“Pia tunatoa fani za Jiolojia, Kemia, Madini, Petroli, Nishati Mbadala, Elimu, lugha, Uhusiano wa Kimataifa, ikolojia, Uandishi wa Habari na Mahusiano ya Umma, fizikia,  na nyinginezo. Zaidi ya Programu 80 katika ngazi ya Shahada za Awali zinatolewa na UDOM, na kwa ngazi ya Shahada za Umahili (Postgraduate Diploma, Masters & PhD) Programu zaidi ya 56,” amesema Rose.

Rose ameendelea kuwasihi wananchi wa Dar es Salaam, Pwani na mikoa jirani kutembelea maonesho hayo kujifunza na kujiunga na programu mbalimbali za Chuo hicho na kwamba huduma za ushauri ni bure.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles