22.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 14, 2024

Contact us: [email protected]

Mkuu wa Wilaya Serengeti akutana na wazee

Na Malima Lubasha, Serengeti

Mkuu wa Wilaya ya Serengeti mkoani Mara,Kemirembe Lwota,amekutana na wazee kwa lengo la kusikiliza changamoto mbalimbali zinazowakabili pamoja na kujadili maendeleo ya miradi inayotekelezwa akiwataka kuendelea kuhimiza, kudumisha na kuilinda amani wilayani kukemea vitendo vya ukatili katika jamii.

Lwota amefanya kikao jana Septemba 19,2024 katika Ukumbi wa CCM Wilaya ikiwa ni mwendelezo wake wa kukutana na makundi mbalimbali wilayani hapa kusikiliza na kupokea changamoto zao ili kuzitafutia ufumbuzi.

Amesema lengo la kukutana na wazee hao pamoja na wananchi na makundi mengine ni kujitambulisha kwao kisha kuwasikiliza changamoto walizonazo pamoja na kujadiliana maendeleo ya wilaya na taifa kutokana na fedha zinazoletwa na Serikali kutekeleza miradi.

Kabla ya kuzungumza na wazee hao, aliwapa nafasi wao kuongea ambapo wengi walizungumzia suala la kudumisha amani,miradi ya maendeleo, elimu,afya,uharibifu wa barabara, mikopo,changamoto ya maji, maadili kuporomoka katika jamii,mifugo kuingia ndani ya hifadhi ya Serengetihuku wakisisitiza kutembelea vijiji kukutana na wananchi makundi tofauti kusikiliza kero zao kuzitolea majibu kisha kwa kueleza msimamo wa serikali kuhusu changamoto hizo.

Wakizungumzia suala la amani wilayani Serengeti wazee hao walisema kuwa amani iliyopo sasa inatoka na umoja na ushirikiano walionao wananchi uliojengwa na waasisi wa taifa hili miaka 60 iliyopita na kuunganisha makabila yote kuishi kama ndugu huku wakikemea viashiria ya vitendo viovu vina vyotokea kila inapofikia kipindi cha uchaguzi.

“Tunakuomba na tunasema kuwa sisi wazee tupo nyuma yako ukiwa mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama endelee kusimamia suala la amani kwa wilaya yetu wazee tutakuunga mkono watu wanaotaka kuvuruga umoja uliopo tunashauri chukua hatua kwani amani iliyopo sasa ni muhimu ambayo itadumi shwa na kulindwa na wote kwa kushirikiana hii amani kwetu si kitu kigeni tuendelee kuilinda,”Walisema wazee hao.

Baadhi ya wazee waliomba mkuu huyo wa wilaya kutembelea hospitali ya wilaya na zahanati wilayani ili kujiridhisha kuhakikisha madirisha yaliyotengwa kwa wazee yanawahudumia wazee.

Wamesema madirisha hayo yapo lakini hayatekelezi kama ilivyoelekezwa na serikali na kusisitiza mikutano hii ya kukutana makundi mbalimbali vjijini iwe endelevu ili kusukuma maendeleo ya wilaya mbele.

Akijibu changamoto na ushauri uliotolewa na wazee hao amesema atafanya kazi kwa kushirikiana nao akizingatia katiba na sheria za nchi akiwataka kuhakikisha amani inaendelea kudumu na kuwashauri wazee kuwa wazi na kusema ukweli wanapopeleka changamoto zao Ofisini kwake na kuahidi atafanya vikao katika kata zote kuzungumza na wananchi kusikiliza na kutoa majibu ya kero zao kwa kuona uteke lezaji wa miradi kwa kuhimizwa kufanya kazi.

“Haya mafanikio yote yatapatikana kutokana na ushirikiano mtakaonipatia kama Mkuu wa Wilaya nina potekeleza majukumu yangu kuipatia maendeleo wilaya hii kipindi chote nitakachokua wilayani Serengeti nikishirikiana na wananchi wa makundi mbalimbali naomba mnipe ushirikiano kukomesha vitendo vya ukatili visivyotakiwa katika jamii,”amesema.

Katika kuilinda Hifadhi ya Taifa ya Serengeti aliwaonya wananchi wanaoishi kando kando ya hifadhi wa kuingiza mifugo yao hifadhini kutafuta malisho na uwindaji haramu kinyume cha sheria waache mara moja waheshimu sheria zilizopo akiwataka wazee kumsaidia kutoa elimu juu ya umuhimu wa hifadhi hiyo kwa uchumi wa taifa.

Aidha Lwota amewataka watu wanaochunga mifugo ndani ya Mji wa Mugumu na kuharibu mazingira na muonekano kuanza kufuga kisasa lengo la kuzuia hili ni ng’ombe,mbuzi na kondoo wanakula miti iliyopandwa tunataka kuufanya mji huu uwe safi kwani hivi sasa mji unatembelewa na watalii wengi wa ndani na nje na kusisitiza wananchi kuendelea kupanda miti mvua zitakapoanza kunyesha.

Ameeleza kuwa changamoto zilizotolewa na wazee hao wakililalamikia baadhi ya idara za halmashauri amezichukua kuzifanyia kazi atakutakuna na viongozi wa Halmashauri akiwemo Mkurugenzi Mtendaji na wakuu wa idara kujadili masuala yaliyoelezwa na wazee.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles