Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital
Staa wa muziki mwenye asili ya Afrika anayeishi nchini Canada, Director P, ameendelea kujizolea umaarufu kupitia wimbo wake mpya, Beauty Queen. Wimbo huo umeonekana kuvutia mashabiki wengi, hasa kwenye mtandao wa YouTube, na kumfanya Director P kuzidi kung’aa katika ulimwengu wa muziki.
Director P, ambaye ni rapa na mwongozaji wa video za muziki, amewashukuru mashabiki wake kwa mapokezi makubwa ya Beauty Queen.
“Afrika ni nyumbani, na ninapata sapoti kubwa sana kutoka kwa mashabiki wa pande hizo. Ngoma yangu ya Beauty Queen imewagusa wengi wanaopenda rapa kutokana na jinsi nilivyoonyesha ufundi wa kumsifia mwanamke ninayempenda,” alisema Director P.
Ameongeza kuwa anashukuru familia yake, hasa mke wake kipenzi, kwa sapoti kubwa wanayompa kwenye sanaa yake, jambo ambalo linampa nguvu ya kuendelea kufanya makubwa kwenye tasnia ya muziki.