29.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 20, 2024

Contact us: [email protected]

Stars matumaini kibao ikiifuata Kenya

Theresia Gasper -Dar es salaam

KIKOSI cha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, kinatarajia kuondoka leo kwenda Kenya kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa kusaka tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN), unaotarajiwa kuchezwa Jumapili, nchini humo.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Stars ilitoka suluhu na wapinzani wao hao, Harambee Stars.

Akizungumza na MTANZANIA jana, kocha msaidizi wa Stars, Seleman Matola, alisema kikosi hicho kilifanya mazoezi ya mwisho jana asubuhi kwenye Uwanja wa Boko Veteran na jioni katika Dimba la Taifa.

“Tunatarajia kuondoka kesho (leo) jioni, saa kumi, kwenda Kenya, tukiwa tayari kwa mchezo wa marudiano dhidi ya Harambee Stars, tukiwa na matumaini makubwa ya kushinda,” alisema.

Alisema wachezaji wote wapo vizuri, kukiwa hakuna majeruhi, kila mmoja akiwa na morali ya hali ya juu kuhakikisha wanafanya vizuri katika mchezo huo.

Matola alisema licha ya kushindwa kupata matokeo mazuri katika mchezo wa nyumbani, wanaamini watapata ushindi ugenini na kusonga mbele.

Stars inawafuata wapinzani wao hao, huku ikiwakosa nyota wake, Ibrahim Ajib, Aishi Manula na Mudathiri Yahya walioumia na kushindwa kuendelea kuwapo kikosini.

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Etienne Ndayiragije, amewaita Haruna Shamte, Oscar Masai (Azam FC) na kipa Mohammed Yussuph (Polisi Tanzania) kuziba mapengo ya wachezaji hao.

Stars inatakiwa kushinda au kupata sare ya mabao katika mchezo huo dhidi ya Kenya ili iweze kusonga mbele.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles