22.1 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

SPIKA NDUGAI ASIMULIA ALIVYOPIGANIA UHAI WAKE

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

Spika wa Bunge Job Ndugai amesimulia jinsi alivyopigania uhai wake wakati akiwa amelazwa nchini India ambapo amesema kuna kipindi alikuwa akihisi hawezi kuiona kesho.

Spika ameyasema hayo bungeni leo ambapo ameongoza kikao kwa mara ya kwanza mwaka huu tangu arejee, mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu.

“Kuna wakati nilikuwa nikiona kabisa siwezi kuiona kesho, baadhi yenu labda hamjawahi kulazwa hospitali mkiwa mnaumwa sana na kama ukiwa peke yako, halafu ukaona jinsi ambavyo mawazo yanavyokuja na kuzunguka na wakati mwingine kunakuwa na dalili zinaonesha kama vile kesho hakuwezi kukucha.”

Spika Ndugai amesema kuna raha na tabu yake kidogo ambapo hawaombei wabunge hao wapitie katika mambo hayo huku akiwaombea wasipate machungu hayo aliyoyapata ambapo pia amewashukuru wale wote waliomuombea wakati akiwa mgonjwa.

“Niwashukuru wote walioniombea kwani binadamu siyo jiwe lazima kupita katika mapito na kila binadamu ana mapito ambayo anaweza kupitia kulingana na alivyopangiwa.

“Kwa hiyo ukipata msalaba unaubeba kwa amani ninaendelea kumuomba Mwenyezi Mungu msalaba wangu na mimi usiwe mzito sana uwe wa kadri tu.

“Vinginevyo nashukuru tumerudi tupo pamoja na niwashukuru sana wasaidizi wangu hapa mezani Naibu Dk. Tulia( Akson) Chenge (Andrew) Najma (Giga) Zungu (Musa) Katibu na timu yake pamoja na wabunge kwa kipekee kabisa Wapigakura wangu wa Kongwa, nawaomba tuendeleze gurudumu letu.

“Kipekee nimeshukuru Waziri Mkuu, (Kassim Majaliwa), tulikuwa tunawasiliana kipekee alikuwa akinitia moyo sana nilipokuwa kitandani kule,” amesema Spika Ndugai.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles