26.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 11, 2024

Contact us: [email protected]

Soka la sasa ni zaidi ya biashara

PAUL  NA BALE

NA BADI MCHOMOLO,

Nyota wa klabu ya Real Madrid, Gareth Bale amekuwa akishikiria rekodi ya kuwa mchezaji ambayo amesajiliwa kuwa kiasi kikubwa kwa uhamisho wake kutoka klabu ya Tottenham na kujiunga na Real Madrid.

Nyota huyo alijiunga klabu ya Real Madrid mwaka 2013, kwa mkataba wa kitita cha pauni milioni 85.3.

Dau hilo lilionekana kuwa kubwa sana tangu kipindi hicho hicho hadi sasa bado hakuna mchezaji ambaye ameweza kulivuka dau hilo la usajili.

Wengi walijiuliza kwa nini mchezaji huyo amesajiliwa na kiasi kubwa cha fedha wakati uwezo wake sio mkubwa kulingana na thamani yake ya usajili, au kuwashinda baadhi ya wachezaji ambao wana majina mkubwa kwenye soka tofauti na yeye.

Lakini ukweli unabaki kuwa soka sasa ni sehemu ya biashara, hata hivyo wapo ambao wanadai kuwa soka kwa sasa ni zaidi ya biashara kwa kuwa thamani za wachezaji zinazidi kuwa juu tofauti na uwezo wao.

Kwa sasa katika usajili ambao unaonekana kusubiriwa na idadi kubwa ya mashabiki na wapenzi wa soka ni kiungo wa zamani wa klabu ya Manchester United, Poul Pogba ambaye kwa sasa anawindwa na klabu hiyo kwa mara ya pili.

Nyota huyo kwa sasa anakipiga katika klabu ya Juventus, lakini anaonekana kuwa thamani yake ni kubwa kuliko mchezaji mwingine katika kipindi hiki cha usajili.

Uwezo wa Pogba ni mkubwa lakini inaonekana thamani yake imekuwa kubwa zaidi ya uwezo, ila kilichopo sokoni kwa sasa ni jina la Pogba limekuwa bidhaa ambayo inaweza kuuzika sokoni (Brand).

Mchezaji huyo hadi sasa inadaiwa kuwa thamani yake ni pauni milioni 100, ambapo thamani ya mchezaji huyo ni kubwa kuliko mchezaji yeyote yule duniani katika dirisha hili la usajili, wakati mchezaji huyo ana umri wa miaka 23.

Wakati mchezaji huyo anaachwa na klabu ya Manchester United, klabu hiyo ililipwa kiasi cha pauni 800,000 kutoka kwa klabu ya Juventus ya nchini Italia huku mchezaji huyo akiwa na umri wa miaka 19, lakini kwa sasa anaonekana kuwa Lulu kwa United.

Mbali na Pogba thamani yake kuonekana kuwa juu, lakini kuna wachezaji wengine ambao wanawindwa na klabu mbalimbali, pia dau zao zinaonekana kuwa juu ikiwa na maana kuwa soka la sasa ni biashara.

Fedha ambayo anatakiwa kuuzwa mchezaji huyo inaweza kuwanunua wachezaji zaidi ya wawili na wakatoa mchango mkubwa katika Ligi na michuano mingine tofauti na vile ambavyo Pogba angetoa mchango wake.

Mshambuliaji wa klabu ya Napoli, Gonzalo Higuain, kwa sasa anawindwa na klabu ya Juventus ambapo klabu hiyo imedai kuwa ipo tayari kuweka mezani kitita cha pauni milioni 78.

Uwezo wa Higuain sio mkubwa sana na kufikia thamani ya fedha hizo, lakini sasa soka ni biashara hivyo mchezaji yeyote anaweza akapewa thamani kubwa tofauti na uwezo wake.

Hata hivyo umri wa Higuain kwa sasa ni mkubwa ana umri wa miaka 28, lakini klabu ambayo itakuwa tayari kumsajili mchezaji huyo itajua jinsi gani ya kurudisha fedha hizo kupitia mchezajin huyo.

Hata hivyo klabu ya Manchester City nayo imeonesha nia ya kuitaka saini ya beki wa kati wa klabu ya Everton, John Stones, ambapo klabu hiyo ya Everton imedai kwamba ipo tayari kumuuza mchezaji huyo kwa kitita cha pauni milioni 50.

Inadaiwa kwamba wachezaji wengi Ulaya thamani yao inakuwa kubwa kutokana na klabu nyingi kuonesha nia ya kutaka kumsajili, hivyo wakala wa mchezaji huyo anazigonganisha timu hizo na bei kuwa kubwa.

Hivyo ndivyo soka la kisasa linavyo endeshwa, na tunatarajia kuona makubwa katika kipindi hiki cha usajili kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu, na inawezekana hali hii inaendelea kwa misimu mingine mingi ijayo.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles