23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Sita wafukuzwa kazi kwa vyeti feki Masasi

FAKENa FLORENCE SANAWA, MASASI

HALMASHAURI ya Wilaya ya Masasi, Mkoa wa Mtwara, imewafukuza kazi watumishi sita waliokutwa na vyeti feki wakati wa uhakiki.

Taarifa hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, Satmah Juma alipokuwa akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani la wilaya hiyo.

Kwa mujibu wa Juma, watumishi hao baada ya kujua uhakiki wa vyeti umeanza kama Serikali ilivyoagiza, waliacha kuja kazini bila taarifa.

“Baada ya taarifa za uhakiki wa vyeti kutolewa, watumishi hao walianza utoro kazini hali ambayo ilitia shaka na vyeti vyao vilipochunguzwa, vilionekana ni feki.

“Kwa hiyo, baraza la madiwani baada ya kukaa kama kamati, limefikia uamuzi wa kuwafukuza watumishi hao sita baada ya kukosa sifa za utumishi wa umma,” alisema Juma.

Alizitaja idara walizokuwa wakifanyia kazi watumishi hao kuwa ni elimu, afya na utawala.

Pamoja na kufukuzwa kwa watumishi hao, mwenyekiti huyo wa halmashauri alisema kamati yake imeagiza wahusika wafikishwe mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles