25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

SINTOFAHAMU KESI YA VIONGOZI CHADEMA, WADAIWA KUTOFIKISHWA MAHAKAMANI

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Kesi ya viongozi sita wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), akiwamo Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, imeibua sintofahamu baada ya watuhumiwa hao kudaiwa kutokuwapo katika mahabusu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

IMEKUWAJE?

Viongozi hao ambao inaaminika walifikishwa mahakamani hapo tangu saa 11 alfajiri leo Alhamisi Machi 29, kwa ajili ya kusikiliza uamuzi wa dhamana yao kwa magari ya polisi yaliyoingia chini ya ulinzi mkali mahakamani hapo huku watu wengi wakiwamo viongozi mbalimbali wa Chadema wakimiminika mahakamani hapo kusikiliza kesi hiyo.

Ilipofika saa nne ndipo ikagundulikwa kuwa kina Mbowe si miongoni mwa mahabusu waliokuja na magari yaliyotoka Gereza la Segerea, bali watuhumiwa wa Kundi la Uamsho wanaokabiliwa na kesi ya ugaidi ambao kesi yao ilitajwa na kasha kuondoka kwa magari hayo hayo

Baadhi ya mawakili mahakamani hapo wamepigwa na butwaa wasijue cha kufanya kwani walijua watuhumiwa hao wako mahabusu ya mahakama hiyo wakisubiri kesi hiyo.

Viongozi wakuu wa chama hicho, Waziri Mkuu wa zamani na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa na Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye, ni miongoni mwa watu waliofika mahakamani hapo lakini wameondoka muda mfupi uliopita kuelekea katika mazishi ya mmoja wa waasisi wa chama hicho, Victor Kimesera, aliyefariki Machi 24 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Pamoja na Mbowe, viongozi wengine ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Vincent Mashinji, Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko ambao wanakabiliwa na mashtaka manane yakiwamo kuhamasisha maandamano, uchochezi na uasi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles