23.9 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Sinema mume wa Shamim kudakwa dawa za kulevya

Na AZIZA MASOUD – Dar es Salaam

MAMLAKA ya Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imesema mfanyabiashara Abdul Nsembo maarufu kama Abdukandida ni papa (kinara) katika mtandao wa biashara ya dawa hizo na anajulikana katika nchi mbalimbali zikiwamo Brazil na Marekani.

Nsembo aliyekamatwa na DCEA Mei Mosi, mwaka huu usiku wa manane akiwa amejificha juu ya dari nyumbani kwake Mbezi Beach, Dar es Salaam, anaendelea kushikiliwa na mke wake Shamim Mwasha kwa kudaiwa kukutwa na gramu kati ya 560 hadi 700 za heroin zilizopatikana baada ya kupekuliwa nyumbani kwao kwa muda wa saa sita kuanzia saa nane usiku hadi saa moja asubuhi.

Akizungumza na MTANZANIA Jumapili katika mahojiano maalumu kwa njia ya simu, Kamishina wa Operesheni wa DCEA, Luteni Kanali Fredrick Milanzi, alidai Nsembo ni miongoni mwa wafanyabiashara wakubwa wa dawa za kulevya waliokuwa wakiwachunguza na kuwatafuta kwa muda mrefu.

“Nyinyi mnamuona Nsembo ni mtu mdogo, Nsembo si mdogo katika mtandao wa dawa, ana network (mtandao) kubwa, ukiwauliza wenyewe watakwambia ni mjanja na amekuwa akifanya biashara hii kwa muda sasa, na huyu kijana pia tuliomkamata juzi sio mdogo ni mkubwa, yeye ndio anatumiwa na wakubwa, hawa watu kuwakuta na kilo mbili tatu si kitu cha ajabu, ingekuwa tunawakuta na gramu tatu mbili ndiyo tungesema wadogo,” alisema. 

Milanzi alisema kupitia biashara hiyo, Nsembo tayari yupo katika mitandao ya kimataifa inayo…

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles