22.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 31, 2023

Contact us: [email protected]

Simu yamwokoa Bob Junior katika ujambazi

Bob JuniorNA SUZANA MAKORONGO (RCT)

UNAWEZA kusema kwamba mitandao ya simu ndiyo iliyomwokoa msanii na prodyuza wa muziki nchini, Rahim Nanji (Bob Junior) katika tuhuma za kuhusika na ujambazi wa kuteka.

Mitandao hiyo imetumika katika uchunguzi wa simu ya prodyuza huyo kama kweli amewasiliana na mtu anayedaiwa kutekwa na msanii huyo baada ya kutoweka kwa muda nyumbani kwake na kumwachia hofu mke wake.

“Nashukuru simu imeniokoa maana nilipokamatwa na polisi kituo cha Magomeni kwa tuhuma za ujambazi niliwekwa ndani siku mbili, ndugu zangu walikuja kunidhamini tukaenda kwenye mitandao ya simu, simu yangu ikachunguzwa ikagundulika kwamba sijahusika na suala hilo.

“Imekua kawaida kwa sisi watu wenye majina makubwa kusingiziwa mambo ili tuonekane tunaishi kwa kuiga, hayo niliyosingiziwa ni chuki tu ambazo hata sijui kwanini zimefanyika hivyo, nami kwa sasa naomba jambo hili liishe ili niwashtaki kwa kunidhalilisha,” alieleza Bob Junior.

Aliongeza kwa kuwataka wenye nia mbaya kwake waache kumsingizia kwa kuwa hakuna binadamu anayejua hatima yake hivyo waishi kwa amani na kupendana huku wakishirikiana badala ya kuchukiana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,205FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles