27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Isihaka sasa kifungo mwezi mmoja, atemwa unahodha

HASSAN-ISIHAKA-800x635NA THERESIA GASPER, DAR ES SALAAM

UONGOZI wa Klabu ya Simba umempunguzia adhabu beki Hassan Isihaka kutoka muda usiojulikana hadi mwezi mmoja huku ukimuondoa katika nafasi ya nahodha msaidizi kutokana kuonesha utovu wa nidhamu kwa kocha wa timu hiyo, Jackson Mayanja.

Adhabu ya kusimamishwa mwezi mmoja kwa Isihaka itaanzia tarehe aliyokabidhiwa barua, ambapo sasa zimebaki siku 11 huku akilipwa nusu mshahara.

Uamuzi huo umefikiwa baada ya Mayanja kuzungumza na Kamati ya Utendaji ambayo ilitoa adhabu hiyo ili beki huyo wa kati aweze kupunguziwa adhabu.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Haji Manara, alisema Simba ni timu kubwa hivyo haiwezi kukumbatia vitendo vya utovu wa nidhamu vitakavyofanywa na wachezaji wake.

“Kocha aliiomba Kamati ya Utendaji impunguzie adhabu, jambo ambalo limekubaliwa na sasa mchezaji huyo atasimamishwa kwa mwezi mmoja na pia ameondolewa kuwa nahodha msaidizi ili iwe fundisho kwa wengine,” alisema.

Alisema wachezaji wanatakiwa kufanya vitendo vinavyoendana na hadhi ya klabu hiyo kwani hawatamuonea huruma yeyote ambaye atakwenda kinyume hata kama kiwango chake kipo juu.

Isihaka ambaye ni mmoja wa mabeki muhimu ndani ya kikosi cha Simba, alikumbwa na adhabu hiyo baada ya kumtolea Mayanja maneno yaliyoashiria utovu wa nidhamu wakati timu hiyo ikijiandaa na mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Singida United.

Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji na Wanachama wa klabu hiyo, Iddy Kajura, alielezea maandalizi ya mchezo wao dhidi ya Coastal Union huku akitamba kuwa wamejipanga kuondoka na pointi tatu ili kuondoa dhana ya kuitwa wa mchangani.

“Tunawaomba mashabiki wa Simba wajitokeze kwa wingi kushuhudia mchezo huo, kwa wale ambao watahitaji usafiri kwenda Tanga kutakuwa na mabasi ambayo kila mmoja atatakiwa kiasi cha shilingi 25,000 kwa nauli ya kwenda na kurudi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles