25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Simiyu wasema corona haijavuruga mipango yao ya kuongoza katika mitihani ya taifa

Na DERICK MILTON-SIMIYU

WAKATI shule za msingi na sekondari zikiwa bado zimefungwa kutokana na mlipuko wa virusi vya corona (COVID -19), Mkoa wa Simiyu umejinasibu kufanya vizuri zaidi katika mitihani ya mwaka mwaka huu.

Mkoa huo umesema licha ya shule kuendelea kufungwa, haiwezi kuwa sababu ya kuwazuia kutimiza malengo yao ya kushika nafasi tatu za juu kwenye mitihani yote ya  taifa.

Katibu tawala wa Simiyu, Jumanne Sagini, akifungua kikao kazi cha viongozi elimu kutoka halmashauri sita za mkoa huo alisema corona haiwezi kuwa sababu ya mkoa huo kushindwa kufikia malengo.

Alisema  licha ya uwepo wa virusi hivyo, walitafuta mbinu mbadala ya kuhakikisha wanafunzi wanaendelea kujifunza.

Alisema kupitia mkakati mpya wa kuwafundisha wanafunzi kwa njia ya mtandao na kutuma maswali nyumbani kwao, wana uhakika lengo la mkoa huo kushika nafasi ya kwanza hadi tatu litafikiwa bila ya vikwazo.

Alieleza mkakati huo ambao umekuwa shirikishi, umefanikisha kuwafikkia wanafunzi wengi hasa wale wa madarasa ya mitihani ya kitaifa shule za msingi na sekondari.

“Hatuwezi kusingizia corona ikiwa tutashindwa kufikia lengo letu, tulizindua mkakati wa kuhakikisha wanafunzi wanaendelea kusoma na umetekelezwa vyema, tuna uhakika mkoa utaendelea kufanya vizuri,” alisema Sagini.

Awali Ofisa Elimu Mkoa, Erenest Hinju, alisema lengo la kikao hicho ni kujadili kwa pamoja utekelezaji wa mkakati mpya wa elimu uliozinduliwa wakati wa kipindi hiki cha corona.

Hinju alisema mbali na kuangalia utekelezaji wake, wanahakikisha wanaweka mikakati zaidi pale ambapo kuna changamoto ili kuweza kufikia lengo lao.

Alisema utekelezaji wa mkakati huo, umekuwa ukitekelezwa vizuri, kwani walimu wameendelea kutuma maswali kwa wanafunzi kupitia kwa wazazi wao ikiwa pamoja na kuunda makundi ya whatsapp kwa ajili ya kufundisha.

Baadhi ya mofisa taaluma wa halmashauri walisema mkakati huo umewasaidia walimu kuendelea kuwafundisha wanafunzi wa madarasa ya mitihani ambapo zaidi ya asilimia 70 wameweza kufikiwa.

“ Katika Halmashuari ya Mji wa Bariadi, walimu wetu wa madarasa ya mitihani wameunda group la whatsapp na wamewafikia wanafunzi karibia wote na kuwapatia maswali na kusahihisha, hivyo lazima mkoa ushike nafasi tatu za juu,” alisema Peter Mosha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles