26.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 28, 2023

Contact us: [email protected]

Simbachawene atumbua wawili

ChaweneNa ELIUD NGONDO, ILEJE

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene, amewatumbua maofisa elimu wawili katika mikoa ya Songwe na Mbeya.

Watumishi hao walichukuliwa hatua baada ya kudaiwa kushindwa kusimamia uendeshaji wa Shule ya Sekondari Ileje na kusababisha wanafunzi kadhaa wa kidato cha tano na sita kulala chini.

Waliotumbuliwa ni Ofisa Elimu, Mkoa wa Mbeya, Mwalimu Charles Mwakalila na Ofisa Elimu Sekondari, Wilaya ya Ileje, Mkoa wa Songwe, James Milanzi ambao wote wanatuhumiwa kutoisimamia vizuri shule hiyo.

Simbachawene alichukua uamuzi huo juzi baada ya kubaini zaidi ya wanafunzi 400 wa kidato cha tano na sita shuleni hapo, walilazimika kulala wawili wawili huku wengine wakilazimika kulala chini kutokana na uhaba wa vitanda.

Wakati akichukua hatua hiyo, waziri huyo alisema amesikitishwa na kitendo cha viongozi hao kupokea wanafunzi wengi vyumba havitoshi hali iliyosababisha kutokea kwa uhaba wa vitanda na miundombinu mingine muhimu.

Kwa mujibu wa Simbachwene, Mwakalila ndiye aliyekuwa anasimamia shule zote za Mkoa wa Songwe wakati wanafunzi hao wanapokelewa kipindi ambacho Songwe ilikuwa sehemu ya Mkoa wa Mbeya kabla haujagawanywa.

“Haiwezekani wanafunzi walale chini wakati viongozi wapo, sasa naagiza mamlaka zinazohusika kumsimamisha ofisa elimu wa Mkoa wa Mbeya ambaye ndiye alikuwa anasimamia mikoa yote miwili na ofisa elimu wa Wilaya ya Ileje kwa upande wa sekondari naye asimamishwe ili kupisha uchunguzi.

“Baada ya ofisa elimu wa Mkoa wa Mbeya ambaye alitakiwa amfuate mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Ileje, lakini kwa kuwa ni mgeni, hatutaweza kumchukulia hatua yoyote na badala yake hawa maofisa ndio wanawajibika,” alisema Simbachawene.

Katika hatua nyingine, Simbachawene alisema ana wasiwasi na taarifa zinazoonyesha kuwa mikoa yote nchini imemaliza tatizo la uhaba wa madawati na kwamba Serikali itaendelea kufanya uchunguzi ili kubaini kujua kama kuna maeneo ambayo bado wanafunzi wanakaa chini.

Wakati Simbachawene akilalamikia wanafunzi kulala chini na kulala wawili wawili, taarifa zilizopatikana zinasema Shule ya Sekondari Ileje ina uwezo wa kusajili wanafunzi wa bweni 200 wa kidato cha tano na sita, lakini mwaka huu imeongeza idadi ya wanafunzi na kusajili 409.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles