22.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 17, 2024

Contact us: [email protected]

Mwinyi ashauri utafiti zaidi ugonjwa wa moyo

mwinyi1bcNa Patricia Kimelemeta, Dar es Salaam

RAIS Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, amewataka wataalamu wa afya kufanya utafiti zaidi wa matibabu ya ugonjwa wa moyo.

Alisema hatua hiyo inaweza kurahisisha utoaji wa matibabu ya ugonjwa huo nchini.

Mwinyi alikuwa akizungumza kwenye uzinduzi wa Hospitali ya JPM,   mtaa wa Kagera   Dar es Salaam jana.

Alisema  kupatikana kwa dawa za wagonjwa wa moyo kutasaidia kupunguza gharama za matibabu nchini.

Idadi ya wagonjwa wa maradhi hayo inaongezeka siku hadi siku  jambo ambalo limewafanya watalaamu kuhangaika  waweze kupata tiba itakayowasaidia wagonjwa hao.

“Maradhi ya moyo ni miongoni mwa maradhi yanayowasumbua wananchi wengi hivyo basi watalaamu wanapaswa kufanya utafiti   waweze kupata tiba ambayo itawasaidia wagonjwa hao,” alisema Mwinyi.

Alisema kwa sababu hiyo,  wadau wa afya wanapaswa kushirikiana na serikali  kuhakikisha   suala hilo linafanikiwa.

Lengo la wananchi ni kupata huduma bora ya matibabu kwa gharama nafuu, alisema.

Aliwataka wamiliki wa hospitali hiyo kutoa huduma ya gharama nafuu ili wananchi wasio na kipato kikubwa waweze kwenda  hospitalini hapo kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Ameir Binzoo, alisema  hospitali hiyo itatoa huduma bora ya afya na kwa gharama nafuu ili kukidhi mahitaji ya wananchi.

“Lengo letu ni kuhakikisha  tunatoa huduma bora ya afya na kwa gharama nafuu  wananchi wengi waweze kujitokeza   kupatiwa huduma ya matibabu, jambo   linaloweza kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali za serikali,”alisema Binzoo.

Aliiomba serikali kushirikiana na hospitali za watu binafsi ili   kubadilishana uzoefu  kusaidia kuwaunganisha katika hospitali za kimataifa kwa ajili ya kupata wafadhili   watakaoweza kuchangia gharama za huduma za matibabu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles