23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

SHULE YAPIGA MARUFUKU SHEREHE ZA KRISMASI

_93032261_turkeyschool

SHULE ya Sekondari Lisesi inayomilikiwa na serikali ya Ujerumani iliyopo nchini Uturuki, imepiga marufuku sherehe za Krismasi jambo ambalo limezua hisia kali nchini Ujerumani licha ya mamlaka ya shule hiyo kukana kuwapo kwa hatua hiyo.

Taarifa hiyo iliyoripotiwa na vyombo vya habari nchini humo jana, ilisema kuwa wafanyakazi wa shule hiyo ya Lisesi iliyopo mjini Istanbul waliambiwa kwamba tamaduni za Krismasi na nyimbo za Carol hazitaruhusiwa shuleni hapo.

Wadau mbalimbali walizungumzia uamuzi huo na kusema kuwa ni wa kushangaza.

Hata hivyo, shule hiyo ilikana kutoa agizo hilo. Shule hiyo inayoitwa Instabul Lisesi ni ya sekondari ambayo imekuwapo nchini Uturuki kwa zaidi ya karne moja na ina takriban walimu 35 wa Ujerumani wanaofadhiliwa na serikali ya Ujerumani.

Wiki iliyopita, uongozi wa shule hiyo uliwatumia barua pepe wafanyakazi wake wakiagiza kwamba hakuna kufanya sherehe na tamaduni za krismasi wala kuimba nyimbo za kuzaliwa kwa Yesu Kristo.

Picha za barua hiyo zilichapishwa na chombo cha Sueddeutsche Ziteung nchini Ujerumani.

Wanasiasa nchini Ujerumani walitoa hisia za kushangazwa na hasira.

Raia mmoja wa Ujerumani mwenye makazi yake nchini Uturuki, ambaye pia ni kiongozi mwenza wa Chama cha Green Party, alisema kuwa hali hiyo inadhirisha kwamba Rais wa Uturuki, Reccep Tayyip Erdogan yuko tayari kuondoa uhuru wa kuabudu kwa kuwa anaamini uongozi wake unatishiwa na nyimbo za Krismasi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles