22.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

UTAFITI: KUJAMIIANA NJIA RAHISI YA KUBORESHA KUMBUKUMBU

3a27b38700000578-3914010-image-a-148_1478541424517

Na Joachim Mabula,

KUNA mengi ambayo tunaweza kufanya ili kuweka akili na ubongo wetu hai na wenye afya bora kadili umri unavyosonga. Kula mboga za majani, kufanya mafumbo ya maneno (crossword puzzles), na kusikiliza muziki ni miongoni mwa shughuli zinazo changamsha ubongo ambazo madaktari hupendekeza.

Sasa, utafiti wa hivi karibuni uliochapishwa katika jarida la “Age and Ageing” (Umri na Uzee) ulibaini kuwa kufanya ngono hadi zaidi ya umri wa miaka 50 kunaweza kuongeza afya ya ubongo, hatimaye kukulinda na ugonjwa wa kichaa cha uzeeni/kupoteza kumbukumbu (dementia).

Kama wanawake wanahitaji sababu nyingine ya kufanya ngono mara kwa mara. Utafiti wa hivi karibuni kutoka Chuo Kikuu cha McGill huko Canada uunasema kujamiiana huimarisha hipokampasi ya mwanamke, sehemu ya ubongo inayohusishwa na kumbukumbu, hivyo, kujamiiana mara kwa mara kunaweza kutoa kuwapa wanawake kumbukumbu bora. Ingawa matokeo ya utafiti huo yana utata, angalau yanatoa motisha ya kisayansi kwa wanawake kufurahia zaidi tendo hilo.

Utafiti umebaini kuwa wanawake ambao hujamiiana kwa kuruhusu uume uingie katika uke (PVI) walikumbuka maneno zaidi walipopewa jaribio la kutambua na kukumbuka maneno, ingawa kujamiana hakukufanya kitu ili kuwasaidia kukumbuka vizuri nyuso, Forbes iliripoti. Kulingana na matokeo hayo, utafiti ulihitimisha kuwa kujamiiana huchochea hipokampasi, eneo la ubongo kwa wanawake linalohusishwa kwa kiasi kikubwa na kumbukumbu ya maneno.

“Kiujumla, matokeo haya ya utafiti yanaonyesha kwamba kujamiiana kwa uume kuingia kwenye uke (PVI) kunaweza kuwa na manufaa katika utendaji kazi wa kumbukumbu kwa wanawake vijana wenye afya bora,” utafiti alihitimisha.

Sasa, kabla hujafikiri kuwa utafiti huu ni moja ya mtego wa kuwafanya wanawake vijana kupenda kufanya tendo la ndoa, utafiti uliopita umeonyesha kuwa aina yoyote ya shughuli ya kimwili iwe ni kutoka mbio au yoga (mfumo wa mazoezi ya maungo na kudhibiti pumzi) ina uwezekano wa kuchochea eneo la hipokampasi. Hii ina maana kwamba si lazima kujamiiana pekee ndio kunasababisha kuongezeka kwa kumbukumbu, ingawa wanawake hushughulika wakati wa tendo lenyewe na kusababisha kuongezeka kwa msukumo wa damu kwenye ubongo.

Hata hivyo, matokeo ni ya kuvutia na yanaonyesha ukweli kwamba ngono inaweza kuwa na faida zaidi mbali na uzazi. Kwa mfano, utafiti wa 2014 uligundua kuwa kufanya mapenzi kunaweza kupunguza wasiwasi, wakati utafiti mwingine uligundua kuwa watu ambao hufanya ngono kwa mitindo mbalimbali (BDSM sex) wana uwezekano mdogo wa kuugua matatizo ya akili (neurosis), wawazi zaidi, wenye ufahamu zaidi, hupatwa na hisia zaidi wanapokataliwa, salama zaidi katika mahusiano yao na walikuwa na ustawi bora kiujumla. Hivyo basi, bila kujali sababu inayokufanya utumie muda wako kimahaba na mtu wako, ni vizuri kukumbuka kujamiiana kuna faida kimwili na kiakili.

Kumekuwa na mkazo kidogo juu ya jinsi ya kufanya ngono katika umri mkubwa kunavyoathiri utambuzi. Bado, tunajua ngono ni sehemu muhimu kwenye masuala ya kijamii, kihisia, kimwili na vipengele vingine kwenye maisha yetu.

Dk. Hayley Wright na Rebecca Jenks wa Chuo Kikuu Coventry walilenga kuchunguza uwezekano wa faida za ngono katika umri mkubwa (uzee).

Watafiti walichambua zaidi ya washiriki 6,800 wenye umri kati ya miaka 50 na 89 kuona ni jinsi gani ngono inavyoathari mchakato wa kuzeeka. Washiriki waliulizwa kuhusu maisha yao ya ngono, ikiwa ni pamoja na kila kitu kuanzia kujichua (punyeto) hadi tendo la ndoa. Mfululizo wa majaribio ulifanyika kuangalia afya ya ubongo ya washiriki.

Katika jaribio la kwanza, washiriki waliombwa kusoma mfululizo wa maneno, kisha kuyakumbuka chini ya mazingira mawili tofauti – mara baada ya kuyasoma na dakika tano baada ya kuyasikia. Jaribio la pili lilihusisha zoezi la mpangilio wa idadi ambapo washiriki walipewa muundo maalumu wa idadi ya namba, kisha kuulizwa kukumbuka tarakimu ambayo iliyopungua/kukosekana (mfano 1, 2, __, 4). Watafiti walizingatia umri, kiwango cha elimu, utajiri, viwango vya shughuli za kimwili, hali ya kinyumba, afya kwa ujumla, huzuni, upweke na ubora wa maisha linapokuja suala la mambo yanayoweza kuathiri shughuli za ngono au utambuzi.

Matokeo ya utafiti yalibaini wale walio jishughulisha na ngono walikuwa na uwezekano zaidi wa kukumbuka kiusahihi maneno na tarakimu kwenye mazoezi ya maneno na namba kuliko wale ambao hawakujishughulisha na ngono. Wanaume walifanya vizuri zaidi kuliko wanawake kwenye baadhi ya majaribio. Wanaume waliokuwa wanafanya ngono walionyesha tofauti kubwa katika alama za ufaulu kwenye majaribio yote kuliko wanawake waliokuwa wanaofanya ngono. Wanawake hawa walifanya maboresho makubwa katika kukumbuka maneno, lakini si namba kwenye mazoezi ya mpangilio wa idadi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,717FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles