24.6 C
Dar es Salaam
Thursday, September 28, 2023

Contact us: [email protected]

SHOTI YA UMEME YATEKETEZA MADUKA

 

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo.

Na JANETH MUSHI-ARUSHA

MADUKA matano yameteketea kwa moto katika eneo la Mianzini mkoani Arusha kutokana na hitilafu ya umeme.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema kuwa tukio hilo limetokea Januari 2, mwaka huu saa 12 asubuhi.

Alisema nyumba hiyo ya biashara inamilikiwa na Emanuel Hagai na Benjamini Hagai, ambapo uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme ambayo ilianzia kwenye majokofu yaliyopo katika Mini Super market ya Mianzini.

“Moto huo umeteketeza maduka matano yaliyopo kwenye jengo hilo na uchunguzi wa awali umebaini chanzo cha moto huo huenda ikawa ni hitilafu ya umeme iliyoanzia kwenye majokofu yaliyokuwepo katika Mini Super market.

“Baada ya moto kuanzia kwenye majokofu ulisambaa kwenye mitungi ya gesi,iliyokua jirani na mitungi hiyo kuanza kulipuka na moto ulisambaa zaidi katika maduka mengine ila mpaka sasa hasara ya mali zilizoteketea haijajulikana ila asilimia kubwa ya mali zimeteketea,” alisema

Kamanda Mkumbo alitumia fursa hiyo kuwaonya baadhi ya wananchi ambao wamekuwa na tabia ya kukimbilia maeneo ambayo moto unatokea, jambo ambalo ni hatari kwa usalama wao.

“Nawaonya baadhi ya wananchi wamekuwa na tabia ya kukimbilia maeneo ambayo moto unatokea, hiyo ina hatarisha usalama wao kwani moto kama wa gesi ni rahisi kulipuka na kusababisha madhara makubwa,”  alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,745FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles