23.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

KAMPUNI YA AIRTEL YATUA SOKO LA HISA DAR

gold-coins-on-bond-market-640-702x336

JOHANES RESPICHIUS-DAR ES SALAAM

KAMPUNI ya simu ya mkononi ya Airtel imeongeza idadi ya kampuni ya tatu kubwa za mawasiliano nchini zilizopeleka maombi ya kujiorodhesha katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Ofisa Mwandamizi wa DSE, Mary Kinabo, alisema  Airtel iliwasilisha maombi hayo Desemba 30, mwaka jana siku moja kabla ya kufika muda ukomo  kutotokana na agizo lililotolewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa.

“Kampuni ya simu yaliwasilisha maombi ya kuuza hisa na kujiorodhesha kwenye soko tangu sheria ilipopitishwa bungeni ni pamoja na Kampuni ya Vodacom, Tigo na Airtel ambayo ilileta maombi Desemba 30, mwaka jana,” alisema Mary.

Desemba 28, mwaka jana Waziri Profesa Mbarawa alizitaka Kampuni zote za simu kuhakikisha zinakamilisha mchakato kuuza asilimia 25 ya hisa kwa Watanzania kama sheria inavyotaka hadi kufikia Desemba 31, 2016.

Profesa Mbarawa, alisema kampuni zilizopata leseni baada ya Julai mosi, mwaka jana kuhakikisha wanatimiza sharti hilo la kisheria kwa kipindi kisichozidi miaka miwili tangu ziliposajiliwa na zisipofanya hivyo zitachukuliwa kupitia kifungu cha 21 (C) cha sheria ya EPOCA, 2010.

Wakati huohuo Mary alitaja kampuni tano ambazo ziliongoza kwa hisa zake kupanda bei katika soko hilo ambazo ni pamoja na ACA kwa asilimia 68.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles