23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Shinikizo kumtaka Ruto ajiuzulu lashika kasi

HUKU mjadala kuhusu vita dhidi ya ufisadi ukizidi kupamba moto, kambi tofauti za kisiasa zikizidi kushambuliana juu ya namna inavyoendeshwa, baadhi ya wabunge wanafi kiria kumng’oa Naibu Rais William Ruto kwa sababu anaipinga.

Wabunge kutoka maeneo ya Mlima Kenya na ukambani wameeleza kughadhabishwa kwao na Dk. Ruto, wakionyesha dalili za kutaka kuwasilisha muswada wa kutokuwa na imani naye.

Wakiwa katika jimbo la Kibunge la Kathiani mwishoni mwa wiki, zaidi ya viongozi 10 walimshutumu Ruto kwa kuiandama Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) namna inavyoendesha vita dhidi ya ufi sadi, wakipendekeza ang’olewe kutoka madarakani.

“Kipengee cha 147 cha Katiba kinasema wewe ni msaidizi wa Rais na ukicheza na kipengele cha 150 kinachoeleza ukifanya hivi na vile, tukakubaini tu, tunakutupa nje, tunakung’oa madarakani,” walisema.

“Serikali ni ya Uhuru, si ya Uhuru na mtu mwingine, Urais haugawanywi, sisi hatuna Rais wawili. Wakati Rais akiwa si mwizi, mwizi yuko kitandani karibu naye,” alisema Mbunge wa Kangema, Muturi Kigano.

Mbunge mwenzake wa Kathiani, Robert Mbui naye alimtaka Rais Kenyatta kumfuta kazi mshirika wake huyo wa karibu zaidi kisiasa, ama awape wabunge fursa ya kumng’oa.

“Ninataka kuuliza Rais, si unajua yule ‘mshirika wa kisiasa wa karibu zaidi’ wako ni nani?

Rudisha huyu mtu nyumbani au tuachie kazi tumng’oe mapema ili ufanye kazi bila vikwazo,” alisema Mbui.

Wabunge hao walikuwa wakizungumza katika hafl a ambayo wabunge wengine kama vile Maina Kamanda (Starehe), Ngunjiri Wambugu (Nyeri Mjini), Paul Koinange (Kiambaa), Dan Mwachako (Wundayi) na aliyekuwa Mbunge wa Dagoretti Dennis Waweru walikuwapo pia.

Viongozi hao walimshutumu Dk. Ruto kuhusu sakata la fedha zinazodaiwa kuporwa kwenye miradi ya mabwawa ya Kimwarer na Arror, kufuatia matamshi yake kuwa si Sh bilioni 21 za Kenya zinazokosekana bali Sh bilioni saba. Waweru alisema,

“Kwa hivyo, hawa wakora wa mabwawa, ambao wanamuogopa DCI wameiba fedha sawa na zile tunazolipia watoto masomo Kenya nzima na kwa hivyo leo tunataka kuwaambia wajiuzulu, kwa sababu wameiba fedha za watoto wetu,” alisema.

Matamshi ya mbunge huyo yaliungwa mkono na Mwachako ambaye alisema yule atakayetajwa kuwa amekula pesa za mwananchi, wacha akae kando uchunguzi ufanyike,”alisema.

Koinange, ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya bunge kuhusu usalama naye alisema pesa zote za umma ambazo zimeporwa zitafi kiwa na kurejeshwa.

Alhamisi, mbunge huyo alikuwa ameitetea ofi si ya DCI, inayoshambuliwa na baadhi ya wanasiasa hasa wa kambi ya Ruto akitaka iongezewe fungu la bajeti ili iimarishe kazi yake.

Seneta wa Siaya, James Orengo alipendekeza Dk. Ruto aondoke serikalini kwa kutofautiana na misimamo ya Rais Kenyatta.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles