30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mueller: Hakuna ushahidi Trump, Urusi kuvuruga uchaguzi

WASHINGTON, MAREKANI

RIPOTI iliyowasilishwa na Mwanasheria Maalumu wa Marekani, Robert Mueller haioneshi uwapo wa ushahidi kuwa timu ya kampeni ya Rais Donald Trump ilishirikiana na Urusi kuhujumu uchaguzi wa Rais mwaka 2016.

Kwa mujibu wa muhtasari wa ripoti hiyo, uliondaliwa na Mwanasheria Mkuu William Barr kwenda kwa kamati ya wabunge wa Baraza la wawakilishi, uchunguzi uliofanywa na Müller haukuthibitisha iwapo Trump alifanya kosa la jinai.

Barr amesema Mueller hakuwa na uhakika iwapo timu ya kampeni ya Trump ilipanga au kuhusika na mpango wa Serikali ya Urusi wa kuingilia kati ya uchaguzi wa Rais wa Marekani mwaka 2016.

Akizungumzia juu ya ripoti hiyo Rais Donald Trump alionesha furaha yake na kusema alijua hana hatia.

Makamu wa Rais wa Marekani, Mike Pence amesema hitimisho la uchunguzi wa Mueller ni uthibitisho wa jumla kuwa Rais Trump na timu ya kampeni wamesafi shwatuhuma mbaya mno.

Amesema hayo ni matokeo muhimu yanayopaswa kupokewa kwa furaha na Wamarekani wanaopenda ukweli na uadilifu uliokuwepo wakati wa uchaguzi.

Pence ameiita siku iliyotolewa ripoti hiyo kuwa ni muhimu kwa taifa la Marekani, Rais Trump na Utawala wake.

Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Urusi Konstantin Kosachev amesema hatua hiyo inatoa fursa ya kuufufua uhusiano kati ya Marekani na Urusi.

Mueller alitumia karibu miaka miwili kuchunguza madai kuwa Urusi iliingilia kati uchaguzi wa urais wa

Marekani na kumsaidia Trump kumshinda mpinzani wake, Hillary Clinton.

Lakini pia mwanasheria huyo mkuu amesema uchunguzi huo haujamwondolea Trump madai ya kuzuia haki kutendeka.

Spika wa Bunge Nancy Pelosi na kiongozi wa shughuli za Bunge Chuck Schumer wote wanachama waandamizi wa Chama cha Democratic wamesema ripoti hiyo inaibua maswali mengi kuliko majibu yaliyopo.

Chama hicho kimetaka ripoti nzima ya Mueller ichapishwe hadharani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles