24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Shigela ataka wananchama Bima ya Afya kupatiwa huduma bora

Na Ashura Kazinja ,Morogoro

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Martin Shigela amewaagiza Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri zote, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Mkoa wa Morogoro, kuendelea kuweka jitihada za kutafuta mbinu mbalimbali za kuongeza idadi ya wanachama wa Mfuko wa Bima ya Afya iliyoboreshwa (iCHF).

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Martine Shigela akimkabidhi mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mathayo Maselle, mkataba wa mpango wa lishe unaotakiwa kutekelezwa kuanzia sasa mkoani Morogoro wakati wa kikao cha nusu mwaka kilicholenga kutathimini mkataba wa mpango wa lishe na Bima ya Afya.

Shigela ametoa agizo hilo leo Jumatatu Julai 19, 2021 kwenye kikao cha nusu mwaka kilicholenga kutathimini Mkataba wa mpango wa lishe na Bima ya Afya ya jamii iliyoboreshwa yaani iCHF kilichofanyika mjini Morogoro mwishoni mwa wiki iliyopita.

Aidha amewataka viongozi hao kuhakikisha zoezi la kuongeza wanachama linaenda sambamba na uboreshaji wa huduma za Afya kwa wanachama wake, ili wanachama hao waone umuhimu wa Kujiunga na Mfuko huo na kuondoa malalamiko yanayotolewa na wanachama kuwa hawapata dawa kupitia Bima hiyo.

‘’Bado Mkoa wetu wa Morogoro tuna changamoto kubwa ya Bima Afya iliyoboreshwa, asilimia kubwa ya wanachama wetu tuliowaandikisha hawapati huduma kama inavyostahili, kumekuwa na malalamiko sana katika upande huu wa Bima, wengi wanalalamika kuwa dawa hakuna wakati sehemu zingine dawa zipo’’ Alisema Shigela.

Kwa upande wake Katibu Tawala mkoa wa Morogoro Mariam Mtunguja, alibainisha kuwa moja ya changamoto inayokabili Mfuko wa Bima ya Afya iliyobereshwa (iCHF) ni kutokuwepo wanachama wa kudumu kutokana na huduma zisizo aminika ambazo hupelekea wanachama hao kutohuhisha bima zao mara tu baada ya kuisha muda wake.

Hata hivyo Mtunguja aliwataka Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Halmshauri zote za Mkoa huo kuwa mstari wa mbele katika kutoa Elimu juu ya faida mbalimbali ambazo zinatokana na (iCHF) ili kuongeza idadi ya wanachama wa kudumu katika mfuko huo.

Awali akiwasilisha taarifa ya Mfuko wa Bima ya Afya Mratibu wa CHF Mkoa wa Morogoro Elicia Mtesigwa, alisema bado wanaendelea na uhamasishaji ili kuyafikia makundi mbalimbali ndani ya jamii ili yajiunge na mfuko huo,  huku akieleza lengo lake sio tu kuwa na wanachma wengi bali kuhakikisha kila mwananchi Mkoani humo anakuwa na uhakika wa kupata matibabu ya Afya wakati wote hata anapokuwa hana fedha mkononi.

Alibainisha kuwa zaidi ya wanachama 56, 000 Mkoani Morogoro wamejiandikisha katika mfuko wa Bima ya Afya iliyoboreshwa kwa mwaka wa fedha 2020/2021 sawa na asilimia 9.5 ya kaya 590,006 ambapo kaya 21, 941 kati ya hizo zinaweza kupata matibabu katika vituo vya kutolea huduma za Afya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles