Shamsa ammwagia sifa JB

Shamsa Ford na JB

NA THERESIA GASPER,

MSANII wa Filamu za kibongo, Shamsa Ford, amefunguka kuwa hakuna mtu anayemvutia kwenye tasnia hiyo kama ilivyo kwa msanii mwenzake, Jacob Steven ‘JB’, kutokana na umahiri wake wa kuigiza.

Akizungumza na gazeti hili jana, Shamsa alisema JB ni mtu mmoja ambaye anajua kugusa uhalisia pale anapoigiza na kukitendea haki kipengele hicho.

“JB anaweza kuigiza kama baba wa familia au kijana na akafiti, vilevile akawapendeza mashabiki wake kutokana na kuigiza kwake, napenda kile ambacho anakifanya,” alisema Shamsa.

Alisema hata anapofanya naye kazi huwa wanatengeneza kitu kizuri ambacho mashabiki wao wanakipokea vizuri.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here