30.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

Wazee Chadema wampinga IGP

Hashimu Issa Juma
Hashimu Issa Juma

NA ESTHER MNYIKA, DAR ES SALAAM

BARAZA la Wazee wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), limelitaka Jeshi la Polisi kuwashtaki waliosababisha maafa na mateso yanayoendelea Zanzibar baada ya kufutwa kwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka jana.

Kauli hiyo imekuja ikiwa ni siku tatu baada ya Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu, kudai jeshi hilo lina ushahidi wa kumkamata na kumfungulia mashtaka Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Baraza hilo, Hashimu Issa Juma, alisema Jeshi la Polisi hadi sasa halijatoa ushahidi huo na kama lina nia ya kupambana na vitendo vya uvunjifu wa sheria ambavyo vinaendelea kutokea Zanzibar, linatakiwa kushughulikia kundi la Mazombi ambalo limekuwa likisumbua wananchi kisiwani humo.

“Wazanzibari wananyanyaswa kwa visingizio vya kuondoa mifugo mjini, watu wanavunjiwa haki zao kwa sababu za kiitikadi.

“Wakati hayo na mengine yakitokea, IGP na jeshi lake wako kimya, kwa nini lakini?

“Wanachokifanya polisi ni kuendelea kutia watu hofu ili wawatawale vizuri, hii si sawa kabisa.

“Kwa hiyo, tunamshauri IGP asiendelee kuwachokonoa Wazanzibari, kwani kufanya hivyo ni kuongeza chumvi kwenye vidonda vibichi,” alisema Juma.

Aliwaomba wazee wote nchini bila kujali itikadi za vyama vyao, waendelee kupigania utawala wa sheria na demokrasia kwani amani itakapotoweka, watu wengi wataathirika.

Kuhusu uongozi wa Serikali ya awamu ya tano, alisema kuna baadhi ya mambo wanamuunga mkono Rais Dk. John Magufuli na kuna baadhi ya mambo hawakubaliani naye.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles