31.2 C
Dar es Salaam
Saturday, December 2, 2023

Contact us: [email protected]

SHAHIDI: VIPIMO VILIONYESHA MANJI ANATUMIA DAWA ZA KULEVYA

Mashahidi wawili wa serikali kutoka Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, wameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu vipimo vya Mkemia Mkuu wa Serikali vilionyesha kuwa mfanyabiashara Yusuph Manji anatumia dawa za kulevya huku Askofu Josephat Gwajima akiwa hatumii.

Shahidi wa kwanza ambaye ni Naibu Mpelelezi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Ramadhan Kingai amedai mahakamani hapo kuwa baada ya watuhumiwa hao kutajwa kwenye orodha ya wanaojihusisha kutumia dawa za kulevya, ofisi yake iliwahoji na kuwapeleka  Kwa mkemia mkuu wa serikali ili kuwapima.

“Baada ya kupimwa majibu yalionesha kuwa Manji anatumia dawa za kulevya aina ya benzodiazepine na Gwajima hatumii aina yoyote ya dawa za kulevya.” Amedai. Shahidi huyo.

Shahidi huyo pia amedai mara baada ya Manji kukutwa anatumia dawa hizo, ofisi yake iliandaa jalada la mashtaka ya kutumia dawa za kulevya na kuipeleka Kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Kwa ajili ya kufunguliwa mashtaka.

Manji alifikishwa mahakamani hapo Februari 16, mwaka huu akidaiwa kutumia dawa za kulevya aina ya heroin.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles