23.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 27, 2024

Contact us: [email protected]

CONTE AKIPIGIA SALUTI KIKOSI CHAKE

LONDON, England

KOCHA wa Chelsea, Antonio Conte, amekisifia kikosi chake kutokana na kazi nzuri waliyoifanya kwenye mchezo dhidi ya Tottenham ambao walishinda kwa  mabao 2-1.

Kutokana na ushindi huo, Conte alimwonya kocha wa wapinzani wao hao, Mauricio Pochettino, kwamba watarajie kipigo kila watakapokutana kwenye Uwanja wa Wembley.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu England, walipata ushindi wao wa kwanza baada ya kuambulia kichapo dhidi ya Burnley wakiwa katika uwanja wa nyumbani.

Mbali na mwanzo mbaya wa ligi hiyo lakini Chelsea walipambana na kuhakikisha wanapata ushindi kwenye mchezo huo.

“Nimewaona vijana wangu wakipambana leo (juzi), kwa hakika nimeona wachezaji wakiwa na hari ya upambanaji jambo ambalo si rahisi kwetu katika kipindi kama hiki ambacho tunakabiliwa na majeruhi. Usisahau Eden Hazard  hakuwepo, licha ya ushindi huu ugenini.

“Kuna kipindi tulipoteana katika mchezo huo, lakini ni jambo la kawaida. Nafikiri tumeonesha kwa wapinzani wetu kwamba sisi kila siku ni hatari. Husisahau kwamba msimu uliopita baada ya kushinda mechi 13 tulipoteza dhidi ya Tottenham kwa kipigo cha mabao 2-0.

“Kwenye ulinzi tumefanya mabadiliko  ya David Luiz  na Gary Cahill, nafasi zao zilichukuliwa na wachezaji chipukizi,  Andreas Christensen na  Antonio Rudiger, hata hivyo tumeonesha kwamba tunaweza,” alisema Conte.

Conte aliusifu Uwanja wa Wembley akidai kwamba hali ya hewa ni nzuri. “Kuwa na hali ya hewa kama hii ni vizuri kwa wapinzani wako,” alisema Conte.

Naye Pochettino, hakuamini kilichotokea akisisitiza kwamba hana haja ya kurudia kuzungumza kilichotokea uwanjani hapo.

“Nafikiri leo ilikuwa wazi, kama unapenda soka na kulitazama utahitaji kuangalia tena mchezo huu kwa kuwa Wembley si tatizo.

“Tulicheza vizuri na kutengeneza nafasi za kufunga lakini hilo ndilo soka, tunatakiwa kukubaliana na matokeo,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles