30.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

WATU WANNE WASHITAKIWA KWA KULA NYAMA YA MTU

Wanaume wanne wamefikishwa kwenye Mahakama ya Afrika Kusini kujibu mashtaka ya ulaji nyama ya binadamu, baada ya madai kuwa mmoja wao alifika katika kituo cha polisi na kusema kuwa amechoka kula nyama ya binadamu.

Alipohojiwa zaidi mwanamume huyo alionyesha sehemu ya mguu na mkono wa binadamu.

Kisha polisi wakafuatana na mwanamume huyo hadi kwenye nyumba moja iliyo mtaa wa KwaZulu-Natal, ambapo sehemu zaidi za miili ya binadamu zilipatikana.

Wanaume hao wanne ambao wawili kati yao ni waganga wa kienyeji, walikamatwa na kushtakiwa kwa mauaji au kupanga kuua.

Walifikishwa katika Mahakama ya Estcourt iliyopo kilomita 175 kaskazini magharibi mwa mji wa Durban.

Msemaji wa polisi aliliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza la BBC kwamba inawezekana kwamba vijana hao wanne, wenye umri kati ya miaka 22 na 32, ni sehemu ya mtandao mkubwa wa watu wanaojihusisha na suala hilo.

Hata hivyo, uchunguzi bado unaendelea na polisi wamewashauri watu ambao jamaa zao wametowewa kujitokeza.

Wachunguzi wa visa vya uhalifu wameitwa kutambua sehemu hizo za binadamu, kwa kuwa haijulikana ikiwa sehemu hizo ni za mtu mmoja au watu kadhaa.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles